Posts

Showing posts from December, 2017

WANANCHI WACHANGIA MAJI NA MIFUGO KUTOKANA NA UHABA WA MAJI KIJIJI CHA NYARUYEYE MKOANI GEITA

Image
Wakazi takribani elfu sita mia tano (6500) wa kijiji cha Nyaruyeye kata ya Nyaruyeye mkoani Geita wanakabiliwa na uhaba wa maji hali ambayo imewalazimu kuchangia maji ya kwenye dimbwi na mifugo. kijiji hicho kina jumla ya visima viwili hivyo wananchi hulazimika kuamka saa nane usiku kwa ajili ya kwenda kupanga foleni. Wananchi wa Kijiji cha Nyaruyeye mkoani Geita wakiwa wanasubiri kuchota maji 

MWANAFUNZI DARASA LA SITA AFUMANIWA AKIWA NA MWANAUME NDANI YA CHUMBA CHAKE MKOANI GEITA

Image
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kamena mkoani Geita amefumaniwa akiwa na mwanaume ndani ya chumba chake. Tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku katika kitongoji cha Bukoba kijiji cha Kamena mkoani humo ambapo mama mzazi wa mtoto huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amethibitisha kutokea tukio hilo na kusikitishwa zaidi huku akilaani vikali kitendo cha mtoto wake huyo mwenye  umri wa miaka 14 kujihusisha na mapenzi badala ya kujikita na masomo ambayo yatamsaidia baadae katika maisha yake.  Nae mwenyekiti wa kitongoji cha Bukoba bwn, James Elias amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuiomba serikali kuwakamata na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaowarubuni wanafunzi kujihusisha na mapenzi.    Na Emmanuel Twimanye.

WAZAZI WAHIMIZWA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO WILAYANI SENGEREMA

Image
Wazazi wameombwa kuzingatia  elimu  inayotolewa kuhusiana na  uzazi wa mpango  ili kupunguza ongezeko la watoto wanaoishi maisha duni pamoja  na kulinda afya za akinamama. Hayo ameyabainisha  Muuguzi Mfawidhi wa  hospital ya  wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza  Bi. Kiaruzi Yegela alipozungumza na Radio Sengerema  ofisini kwake   na kusema kuwa ni vyema wazazi  kuzaa idadi ya watoto wanao weza kuwa hudumia. Sambamba  na  hayo Bi. Yegela amewasisitiza  hasa akina mama wajawazito   kufika kwenye vituo vya afya ili kufanyiwa  utafiti wa magonjwa  ya moyo pamoja  na maendeleo ya mtoto  alieko tumboni. Vilevile  Muuguzi huyo  ameongeza kuwa   ni muhimu  wanajamii  kutumia  dawa kwa kufuata  maaelekezo ya wataalamu wa afya. Na Bwiza Boniphace.

WAHUDUMU WA AFYA WANALAZIMIKIA KUISHI NYUMBA ZA KUPANGA KUTOKANA NA UKOSEFU WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA AFYA NDELEMA GEITA

Image
Baadhi ya watumishi wa zahanati ya kijiji cha Ndelema kata ya Kamena mkoani Geita wanalazimika kulala kwenye nyumba za kupanga zilizopo umbali mrefu kutokana na ukosefu wa nyumba za watumishi katika zahanati hiyo kwa zaidi ya miaka 3. Akizungumza na Radio Sengerema Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Bi, Slivia Fabiani amesema kuwa kero hiyo imekuwa ni ya muda mrefu lakini kwa sasa tayari serikali ya kijiji cha Ndelema na serikali ya mkoa wa geita wameanza zoezi la kusomba mawe na mchanga ili kuanza ujenzi wa nyumba za watumishi hao mara moja. Mbali na changamoto hiyo Mganga Mfawidhi ametaja kuwa zahanati hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi kwani kwa sasa kuna watumishi watatu pekee hali ambayo inapelekea kufanya kazi bila kupata muda wa kupumzika sambamba na kushindwa kumudu kuwahudumia wagonjwa kwa wakati.  Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa upungufu wa watumishi katika zahanati hiyo huwalazimu kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa matibab

WANANCHI WATESWA NA UHABA WA MAJI LICHA YA MAJI YA KISIMA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI KIJIJI CHA NYAMILILO SENGEREMA

Image
Wananchi wa kijiji cha Nyamililo kata ya Kasungamile wilayani Sengerema   mkoani Mwanza  wamelalamikia  mradi mpya wa maji ya kisima kushindwa kutoa huduma hiyo kama ilivyokusudiwa hali inayopelekea  wananchi kuendelea  kukabiliwa na uhaba wa maji. Hayo yamebainishwa na wananchi walipoongea na Radio Sengerema kijijini hapo wameitaka serikali kumaliza tatizo la mradi wa kisima hicho. Diwani kata ya Kasungamile  Julias Mussa Ndekeja aidha amekiri kuwa toka mradi huo uzinduliwe haujafanya kazi yake ipasavyo hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo linashughulikiwa Mradi wa  kisima kirefu cha maji cha Nyamililo ni miongoni mwa miradi  iliyozinduliwa katika wilaya ya Sengerema kwenye mbio za mwenge mwaka huu ulitegemewa kumaliza tatizo la uhaba wa  maji kwa wananchi wa kijiji cha  Nyamililo. Na Charles Sungura

MAMA WAJAWAZITO WATAKIWA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI ILI WAMNUSURU MTOTO ALIYEPO TUMBONI

Image
Akinamama wajawazito wanatakiwa kuacha kutumia dawa za kienyeji  pindi wawapo wajawazito ili kumnusuru mtoto aliyepo tumboni.   Hayo ameyabainisha Muuguzi Mfawidhi wa hospital  ya segerema Bi Kiaruzi Yegera amewataka akinamama wajawazito kuhudhuria klinik  ili kuachana na matumizi ya dawa za kienyeji pamoja na ushauri mbalimbali. Pia  Bi. Kiaruzi amewataka  akinamama  wote  wakiwemo  watumishi wa umma  na  watumishi wa sekta binafisi  kuzingatia lishe  stahiki  ili kulinda  afya ya mtoto. Hata hivyo, Muuguzi huyo amewasisitiza mama wajawazito wote kufika katika  katika vituo  vya  afya ili kupatiwa elimu sahihi kuhusu madhara ya matumizi ya  dawa  za kienyeji. Na,BWIZA BONIPHACE

SHIRIKA LA ORECORP LAKABIDHI MABATI 138 KATIKA SHULE YA MSINGI IGALULA WILAYANI SENGEREMA

Image
Shirika la ORECORP lakabidhi  mabati  138  yenye thamani ya shilingi  milioni tatu laki nane na hamsini elfu katika shule ya msingi Igalula iliyopo katika kijiji cha Lubungo wilayani Sengerema mkoani Mwanza . Akikabidhi mabati hayo Afisa Mahusiano wa shirika hilo JOHN BWANA  amewapongeza wananchi kwa ushirikiano pamoja na jitihada wanazozionyesha katika shughuli za maendeleo na kukamilisha  ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa. Kwa upande wake diwani wa kata ya Igalula Mh,Onesmo Mussa Mashili ameishukuru kampuni hiyo na kutoa agizo kwa wananchi na viongozi kuwa isitokee mabadiliko yoyote ya matumizi katika misaada  hiyo iliyotolewa. Hata hivyo afisa elimu idara ya shule ya msingi  Bwn PIUS LWAMIMI kwa niaba ya Mkurugezi Mtendaji wa wilaya ya Sengerema  ameishukuru kampuni hiyo kwa misaada wanayoitoa katika miradi ya maendeleo . Bwn .JOHN  ameongeza kuwa ujenzi huo wa madarasa ifikapo mwezi wa kwanza uwe umekamilika ili watoto wapate elimu katika maz

MVUA YA MAWE YAHARIBU ZAIDI YA HEKARI 300 KIJIJI CHA IKANDILO GEITA

Zaidi ya  hekari  300 za mazao mbalimbali  katika kijiji cha Ikandilo Kata ya Nyarugusu Mkoani Geita  zimeharibiwa na Mvua ya mawe  huku  wananchi wa eneo hilo wakihofia kukumbwa na baa la njaa. Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw,Furaha Manyanda   amethibitisha   kutokea kwa  tukio hilo  na    kusema  kuwa Mvua hiyo imeharibu mazao mbalimbali ikiwemo maharage ,Mahindi na Pamba pamoja na baadhi ya nyumba   kubomolewa. Bwn, Manyanda  ameeleza kuwa suala hilo limepelekea wakazi hao kukosa usingizi  wakiwaza  wataweza kwenda na kasi ya msimu wa kilimo  kwa wakati huu ikiwa msimu wa kupanda  baadhi ya mazao umeshapita. Hata hivyo  afisa mtendaji huyo  amewaomba wakulima kuacha kukata tamaa na badala yake walime mazao yanayostahimili ukame ikiwemo mtama,  na mihogo huku akidai kwa wamepanga kuitisha kikao na wakulima ili kujadilia changamoto hiyo.

WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA MIUNDO MBINU YA BARABARA KIJIJI CHA KASUNGAMILE WILAYANI SENGEREMA

Wananchi wa kata ya  Kasungamile wilayani Sengerema  mkoani Mwanza   wametakiwa  kulinda na kutunza  miradi ya maendeleo wakati   serikali inapokamilisha ujenzi wa  miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu. Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Kasungamile Mheshimiwa Julias Mussa Ndekeja kwenye mkutano wa wananchi katika kijiji cha Nyamililo alipokuwa akikabidhi mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyamililo kwenda Bulunga baada ya Halmashauri ya Sengerema kukamilisha  ujenzi  barabara hiyo. Wananchi wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha barabara ya Nyamililo kwenda Bulunga hivyo imeelezwa  kukamilika kwa ujenzi wake kumepelekea  wananchi kuipongeza serikali kwa juhudi   za kuwapatia maendeleo na kuahidi kuendelea   kuiunga mkono.  Na Charles Sungura.

KAMPUNI YA TANGA SIMENT YATOA MSAADA WA MIFUKO MIA SITA KWA AJILI YA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA NYAMATONGO WILAYANI SENGEREMA

Image
Katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha elimu kwa mtoto wa kike nchini,Kampuni ya Tanga Simenti imetoa mifuko mia sita(600) ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari nyamatongo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza. Akizungumza na wananchi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo,iliyofanyika shuleni hapo,Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Tanga Simenti Dr Laurence  Kego Masha amesema kuwa, anaimani kuwa shughuli ya ujenzi itasimamiwa vizuri na kwa umakini zaidi hadi kukamilika na itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Tanga simenti Dkt Laurence Kego Masha mwenye tishet nyeupe katikati akikabidhi mifuko ya saruji kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Mh,Evarist Yanga Makanga wa kwanza kulia Nae, Mwenyekiti wa halimashauri ya Sengerema ambae pia ni diwani wa kata ya Nyamatongo Mh.Evarist Yanga Makaga amesema kuwa,atahakikisha anasimamia saruji hiyo ili itumike kwa male

SERIKALI YAANZA KUPELEKA WAHUDUMU WA AFYA KATIKA ZAHANATI YA KISHINDA WILAYANI SENGEREMA

Image
Kutokana na Radio sengerema kurusha habari ya ukosefu wa  wa hudumu  wa afya   katika zahanati ya kijiji cha Kishinda kata ya Kishinda hatimae serikali imeanza kupeleka wahudumu wa afya katika zahanati hiyo. Wakizungumza na Radio sengerema baadhi ya  wananchi wa kijiji   hicho  wameipongeza radio sengerema kwajitihada walizozifanya katika kuripoti habari iliyopelekea serikali kuchukua hatua. Nae mwenyekiti wa kijiji cha Kishinda MASUMBUKO KAKINDA  ameishukuru Radio sengerema kwakurusha habari zenye tija katika jamii. Kwa upande wake mmoja kati ya  Wauguzi wa kituo hicho BARAKA JACOBO pia ameishukuru Radio sengerema kwakuibua changamoto katika jamii. Radio  sengerema  imerusha    habari ya upungufu wa wahudumu wa afya katika zahanati hiyo  Apiril  mwaka huu ambapo hadi kufikia desemba mwaka huu tayari serikali imechukua hatua  za makusudi  na  kuanza kupeleka wauguzi katika zahanati hiyo. Na Deborah Maisa.

MAMA WAJAWAZITO WA KIJIJI CHA NYAMIZEZE WILAYANI SENGEREMA WAONDOKANA NA ADHA YA KUJIFUNGULIA NJE YA ZAHANATI

Image
Akinamama   wa  kata ya Nyamizeze  Wilayani  Sengerema Wameondokana  na  tatizo  la  kujifungulia  njiani  kwa muda mrefu  kutokana na zahanati hiyo kujenga chumba cha kujifungulia akinamama. Hali hiyo imekuja kufuatia miezi mitano iliyopita Radio Sengerema kuzulu katika zahanati hiyo na kurusha habari inayohusiana na kero hiyo. Wakizungumza na Radio Sengerema  baadhi ya akinamama wa kata hiyo wakionyesha nyuso za furaha  wameishukuru radio sengerema kwa kutumika kama daraja la kuwasaidia kutatuliwa adha hiyo. Suzana  Busasa  Kazimili  ni mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Nyamizeze  anakiri Radio Sengerema  imeleta mageuzi makubwa katika zahanati hiyo kwani   imekabiliwa na ukosefu wa chumba cha kujifungulia kwa muda mrefu. Mganga  Mfawidhi  wa  Zahanati  hiyo  Bi,Zuhura  Ramadhani  ameipongeza  Radio  Sengerema  kwa kurusha habari hiyo na kuleta mafanyikio.  Radio Sengerema imerusha habari ya ukosefu wa chumba cha kujifungulia  akinamama  katika zahan

WAZAZI WATAKIWA KUWAJENGEA MAISHA MAZURI WAKATI WA KUJISOMEA WATOT WAO

Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Afisa Elimu shule za sekondari katika Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza Bwn Godwin Balongo amesema utaratibu wa wanafunzi kupata chakula shuleni wakati wa masomo unatarajia kurejeshwa tena mwaka 2018. Bwana Balongo amesema awali zoezi hilo lilikwamishwa na mwitikio hafifu wa wazazi kuchangia chakula cha watoto wao wakiishinikiza kuwa serikali ya awamu ya tano imeleta neema ya mfumo wa elimu bure hivyo hawakuwa tayari kuchangia. Kaimu Mkurugenzi  huyo ameongeza kuwa kwa mwaka ujao ni wakati muafaka kwa wazazi wote kuzingatia agizo hilo ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki. Bwna Godwin amedai kuwa ikiwa wazazi wataunga mkono suala hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa  kuongeza ufaulu wa wanafunzi.  Na,BWIZA BONIPHACE

PANGA LAMNYANG'ANYA MWENDESHA BODABODA PIKIPIKI YAKE WILAYANI SENGEREMA

Image
Mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda aliyetambulika kwa majina ya  Faida Mathias (18) mkazi wa Tabaruka Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amenusurika kuuwawa baada ya kukatwa na  Silaha    aina ya panga sehemu ya kichwa na watu wasiojulikana. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia decemba 14 mwaka huu ambapo mwendesha bodaboda huyo alikodiwa na mtu ambaye hamfahamu baada ya kufika kwenye Nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Sengerema ndipo amemuamuru asimame na ghafula wametokea watu na kuanza kumshambulia  baada ya hapo wamechukua pikipiki yake nayo kutoweka kusikojulikana. Radio Sengerema imefika hosptali teule ya wilaya ya Sengerema na kuzungumza na Manusura wa tukio hilo   na kusimulia jinsi tukio lilivyo tokea. Nae mkuu wa kitengo cha usalama barabara wilaya ya Sengerema Inspecta Hamis Wembo amefika  sehemu ya tukio na kuahidi kuitisha kikao mara moja cha waendesha bodaboda kwa ajili ya kuweka mikakati ya kutokomeza matukio hayo. Matukio ya waend

UFAULU WA DARASA LA SABA WAONGOZEKA KWA ASILIMIA 6 WILAYANI SENGEREMA

Image
Kutokana na kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba K itaifa  wanafunzi Elfu sita mia tisa themanini na nne (6984) wilayani sengerema  mkoani Mwanza wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mwaka  2018. Akizungumza na Radio Sengerema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Afisa Elimu shule za sekondari wa Halmashauri Sengerema Bw, Godwin Balongo ambapo amebainisha kuwa jumla ya watahiniwa Elfu nane mia nne themanini na tatu(8483) sawa na asilimia 99.2 ikiwa wasichana walikuwa ni Elfu nne mia tatu sabini na sita(4376) na Wavulana walikuwa Elfu nne miamoja na saba (4107) ambapo wanafunzi Elfu sita mia tisa themanini na nne ndiyo wamefaulu kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018. Aidha amebainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 6 ukilinganishwa na mwaka 2016 ambapo ulikuwa asilimia 76.1 na mwaka huu  asilimia 82.3 ikiwa watahiniwa 37 hawakufanya mtihani wavulana wakiwa 29 na wasichana 34 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, mimba za utoto pa

SHULE YA SEKONDARI YAAHIRISHWA KUFUNGULIWA MWAKA 2018

Wananchi wa kata ya Ibisabageni  Wilayani  Sengerema Mkoani Mwanza  wameshangazwa  na  kitendo cha Serikali kutowapanga wanafunzi  wa  kidato  cha kwanza  katika shule  hiyo  licha ya kukamilika kwa  madarasa ya kidato  hicho mwaka huu. Hayo yameelezwa na  wananchi kwenye  kikao cha Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Sengerema CCM Bwn Mark Augustne  Makoye  ambapo wananchi wamesema kufunguliwa kwa shule  hiyo  kutapunguza adha ya wanafunzi  kutembea  umbali mrefu kufuata elimu shule za kata jirani. Kwa upande  wake diwani wa kata hiyo Bwn Jumanne Masunga ameshangazwa shule  hiyo kutopangiwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu licha ya kuwepo kwa madarasa na kwamba walitarajia mwaka 2018 itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza rasmi. Akitolea ufafanuzi kuhusu kutofunguliwa kwa shule hiyo Afisa Mtendaji wa kata ya Ibisabageni  bwn   Adam Salum amesema tatizo ni kwamba haijakamilika kwa maabala  na kuiomba serikali isaidie katika vifaa vya maabala. Ziara ya

BODABODA WATAKIWA KUEPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA SENGEREMA

Image
Madereva pikipiki maarufu bodaboda wilayani Sengerema wametakiwa kuepuka matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo ulevi na kuzingatia elimu wanayopewa na viongozi wa usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara. Hayo yamesemwa na  Mkuu wa usalama barabarani  mkoa wa Mwanza ,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Tanzania Mkadam Hamiss Mkadam ,alipokuwa akizungumza na umoja wa waendesha bodaboda wilayani Sengerema mkoani Mwanza na kudai kuwa ni vyema wazingatie maelekezo yote pamoja na sheria za usalama barabarani Mkuu wa usalama barabarani   mkoa wa Mwanza  Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Tanzania Mkadam Hamisi Mkadam Kwa upande wao waendesha bodaboda wamesema kuwa watatekeleza na kusimamia sheria za usalama barabarani kwa umakini ,ikiwa ni pamoja na kupambana na suala zima la matumizi ya dawa za kulevya. Sambamba na hayo  kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Tanzania Mkadam Hamiss amesisitiza kuwa ni vyema madereva kuzingatia usafi kwa hali ya juu i

UJENZI WA CHOO CHA SHULE YA MSINGI NYAMILILO WILAYANI SENGEREMA WATAKIWA KUKAMILIKA KABLA YA MWAKA 2018

Wananchi   wametakiwa kukamilisha ujenzi wa choo  katika shule ya msingi Nyamililo  kata ya Kasungamile wilayani Sengerema  mkoani  Mwanza kabla kufunguliwa kwa  shule hiyo. Hayo yamebainishwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamililo Bwana Dominic Jile   kwenye mkutano wa wazazi alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya shule hiyo. Kwa  upande  wake  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamililo Bwana Mateso Shibai amewataka wananchi kushirikiana na uongozi katika kukabiliana na changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo ujenzi wa choo. Shule  ya  Msingi Nyamililo  inaendelea kuboresha miundo mbinu  kwa kupanda miti ikiwa ni pamoja na kukarabati madarasa na nyumba za walimu kwa nguvu  za wananchi,mashirika na wafadhili mbalimbali.   Na Charles Sungura.

WANANCHI WATAFUTA SULUHU YA KUTOKOMEZA MBWA WANAOSHAMBULIA MIFUGO WILAYANI SENGEREMA

Image
Wananchi    wa kijiji cha Lugata kata ya Lugata wilayani Sengerema wameiomba serikali ya kijiji  hicho  kutafuta suluhisho la  kuwateketeza  mbwa wote  wanaoshambulia mifungo yao  katika  kijiji  chao. Wakiongea na Radio Sengerema   wananchi    hao       wamesema kuwa tatizo hilo limekuwa ni la muda mrefu bila kupatiwa suluhu ya kudumu huku wakieleza kwa masikitiko namana mbwa hao wanavyoshambulia mifugo yao. Kwaupande wake mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Lugata BW CLAVERY TONGANWA amekiri kuwepo kwa kundi hilo la mbwa katika kijiji hicho. Aidha  mwenyekiti  huyo  ameongeza kuwa wameshatoa taarifa kwa afisa mtendaji wa kata  ambaye amewaruhusu kuwasaka mbwa hao  na  kuwaua.  Na  TUMAINI    JOHN.

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

Image
Wakazi wa kisiwa cha Zilagula kilichopo katika kata ya Bulyaheke halmashauri ya Buchosa   wilayani Sengerema   wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu hususani katika msimu huu wa mvua zinazo endelea kunyesha. Wakizungumza na Radio Sengerema katika kisiwa hicho wamesema mazingira wanayoishi siyo salama kwa afya zao kutokana baadhi ya wakazi  wa eneo hilo kutokuwa na vyoo pamoja Nguruwe kuishi pembezoni mwa ziwa hali ambayo mvua zikinyesha uchafu wote hutiririshwa ziwani.                                                                           Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji katika kisiwa hicho Abushilu Yasini amesema hali ya mazingira ni mbaya hivyo serikali ione umhimu wa kukabiliana na tatizo hilo. Hata hivyo baada ya jitihada za kuzungumza na Bwana Afya huyo kuwa za kukatisha tamaa, Radio Sengerema ikalazimika kumtafuta  mkurugenzi  wa halimashauri ya Buchosa Bwn, Crispin Luanda kwa njia ya simu na simu iliita bila mafanikio n

KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO SHULENI NI MSINGI WA UFAULU MZURI

Walimu wa shule  ya  msingi  Nyamililo kata ya Kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza  wamewataka  wazazi  kufuatilia   maendeleo  ya watoto   shuleni ili  kujua  maendeleo  ya  masomo ya  watoto   wao .       Hayo yamebainishwa  na walimu hao  kwenye kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo  walimu     wamesisitiza ushirikiano kati ya wazazi na walimu katika  kuinua kiwango cha elimu kwa  wanafunzi. Pamoja na Serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure nchini lakini  wazazi wametakiwa kutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha mtoto anaenda shule ikiwa ni pamoja  kumnunulia  sare na vifaa vyote  vinavyohitajika. Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nyamililo   Dominic  Jile amesema kitaaluma shule imeendelea kufanya vizuri katika  mitihani  mbalimbali. Kwa  upande wao  Wazazi wamepongeza kwa mshikamano uliopo kati ya uongozi wa shule na wa  serikali ya kijiji hali iliyopelekea kufanikiwa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na     kutatua changamoto  mbalimbali   

AFIKIKISHWA MAHAKAMANI KISA UBAKAJI NA KUMPATIA UJAUZITO MWANAFUNZI

Image
Mtu mmoja  amefikishwa  katika mahakama  ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza  kwa tuhuma ya makosa mawili likiwemo la ubakaji. Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Monika Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi inspekta Slyvester Mwaiseje amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ibrahim Mohamed mwenye umri wa miaka 22 mkazi  wa Nyehunge  wilayani hapa. Mwaiseje amesema kuwa mshitakiwa anashitakiwa  kwa kosa la kubaka kinyume na kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili [e] na kifungu cha 131 kidogo cha kwanza cha kanuni ya  adhabu ambapo amembaka msichana mwenye umri wa miaka 17 ambae jina lake limehifadhiwa     anaesoma kidato cha pili  wilayani  Sengerema. Mshitakiwa ametenda kosa hilo   Juni  mwaka  huu  majira ya saa 2 usiku katika kijiji cha Nyehunge wilayani humo mkoani  mwanza. Kosa la pili ni kumpatia ujauzito msichana huyo kinyume na kifungu cha 5 cha kanuni ya adhabu ya elimu mwaka 2003 kinachotokana na kifungu cha 35kidogo

WANANCHI MJINI SENGEREMA WAHIMIZWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Image
Wananchi wilayani  Sengerema   Mkoani   Mwanza  wamehimizwa kuzingatia   utunzaji  wa  mazingira kwa  kupanda  miti  hasa  katika  msimu  huu  wa  mvua.   Hayo yamebainishwa  na    Afisa  maliasili   wa Halmashauri ya     Sengerema  Bwn Paul  Ponsian  wakati  akiongea  na  Redio  Sengerema  ofisini  kwake,ambapo  ameeleza  kuwa  kwa  yeyote  anaehitaji  kibari  cha  kukata  mti  ni  lazima  awe  na  miti  isiyopungua  5  ili  kuendelea  kutunza  mazingira. Bwn  Ponsian  ameongeza  kuwa  katika  msimu  huu  miche  iliyooteshwa  ni  milioni  mbili  na  laki  tatu na  iliyopandwa  ni  miche  laki  nane  na  elfu  sitini,  kutoka  vitaru mbalimbali   ikiwemo vya    Nyanchenche,Katungulu,Ibanda, Chamabanda  Bwawani  mazingira   na  kitaru  kilichopo  halmashauri ya Sengerema . Aidha Afisa  huyo  amesema,  wana wataalamu  wa  mazingira  katika  maeneo  mbalimbali  kwa  ajili  ya  kuhakikisha  elimu  ya  upandaji   miti  na  utunzaji  wa  mazingira  inawafikia  watu  kwa  ur

BIA YASABABISHA DEREVA BODABODA KUACHA PIKIPIKI YAKE WILAYANI SENGEREMA.

Image
Dereva     pikipiki   maarufu  kama  Bodaboda  amejeruhiwa   na   kitu   chenye    ncha   kali  sehemu za  mwili  wake   na   kisha  kutelekezwa   pikipiki  yake katika mtaa  wa  Kanyamwanza kata  ya  Mwabaluhi  wilayani  Sengerema. Tukio  hilo  limetokea   usiku wa  kuamukia  Desemba  08 mwaka huu   katika  mtaa  wa kanyamwanza  wilayani  Sengerema. Kwa  upande  wake  kamanda  wa  jeshi  la  sungusungu  katika  mtaa wa  huo   bwn, SIMONI  MPUYA,   amethibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo  na  kusema  kuwa   dereva    pikipiki  huyo   ni wa kituo cha pikipiki cha  Nyanchenche   Road Wilayani humo. Kamanda   Mpuya  amewataka  waendesha  bodaboda   kuwa makini    na  wateja  wao  wanaowabeba   hasa  katika  nyakati  za  usiku  ili kuepukana   na matukio  kama  hayo. Nao   baadhi ya  madereva    pikipiki   wa mtaa wa Kanyamwanza   wamesema  kuwa  hali  ya  matukio  ya  wizi  wa  pikipiki  katika  mtaa huo  kwa sasa     limekuwa  ni  tatizo  la  muda  mrefu  bila  kupat

SIMU ZATAJWA CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI WILAYANI SENGEREMA

Image
Baadhi ya wazazi na walezi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamekemea vikali suala la watoto kumiliki simu wakiwa bado masomoni hususani kwa watoto wa kike ili kuepuka janga la mimba za utotoni . Wakiongea na radio Sengerema kwa nyakati tofauti wamesema kuwa simu ni chanzo kikubwa cha maadili  kumomonyoka  kwa watoto.   Hata hivyo wameongeza kwa kusema kuwa wazazi na walezi wasiwe chanzo cha kupelekea watoto wao kumiliki simu kwani malezi bora yanatoka kwa mzazi na yanahitaji umakini zaidi. Pia wazazi wamewasihi watoto kuzingatia  zaidi  masomo  ili waweze kutimiza   ndoto zao katika maisha na wawe na utii na nidhamu   kwa wazazi ,walezi na walimu. Na Glorius  Balele.

MASOMO YA ZIADA YAONGEZA ULEWA WA WANAFUNZI WILAYANI SENGEREMA

Image
Kutokana na umuhimu wa masomo ya ziada kwa wanafunzi, wazazi na walezi  wilayani sengerema wameombwa kuwapeleka wanafunzi kupata masomo hayo wakati huu wa likizo ili wajiendeleze   kimasomo. Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu walipo zungumuza  na Radio Sengerema na kusema kuwa ni vyema  wazazi wakawaendeleza kimasomo  wanafunzi  wawapo nyumbani ili kuwajengewa uelewa  zaidi .     Nao baadhi ya wanafunzi    wamesema kuna  umuhimu  mkubwa  kupata    masomo  hayo   ya  ziada wakati wa  likizo  kwani  yatawajenga    kitaaluma. Sanjari na hayo  walimu hao  wameongeza kuwa   wazazi na walezi  wanajukumu la kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ikiwemo kupitia madaftari   yao   kila watokapo  shuleni ili kujua maendeleo yao.  Na Ester Mabula.