KAMPUNI YA TANGA SIMENT YATOA MSAADA WA MIFUKO MIA SITA KWA AJILI YA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA NYAMATONGO WILAYANI SENGEREMA
Katika
kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha elimu kwa mtoto
wa kike nchini,Kampuni ya Tanga Simenti imetoa mifuko mia sita(600) ya Saruji
kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari nyamatongo
Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Akizungumza
na wananchi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo,iliyofanyika shuleni
hapo,Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Tanga Simenti Dr Laurence Kego Masha amesema kuwa, anaimani kuwa
shughuli ya ujenzi itasimamiwa vizuri na kwa umakini zaidi hadi kukamilika na
itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Tanga simenti Dkt Laurence Kego Masha mwenye tishet nyeupe katikati akikabidhi mifuko ya saruji kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Mh,Evarist Yanga Makanga wa kwanza kulia |
Nae,
Mwenyekiti wa halimashauri ya Sengerema ambae pia ni diwani wa kata ya
Nyamatongo Mh.Evarist Yanga Makaga amesema kuwa,atahakikisha anasimamia saruji
hiyo ili itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Evarist Yanga Makaga akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa Msaada huo na Kampuni ya Tanga simenti |
Kwa
upande wake Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Sengerema,ambae ni Katibu Tarafa ya
Katunguru Bwn Batalangile Malango Kaswahili amesema kuwa,ujenzi huo utaanza mara
mja tarehe 27/12 mwaka huu, na kuagiza watendaji kusimamia sementi hiyo na
kwamba wachukuliwe hatua kari za kisheria wale wote watakao bainika kuiba na
kukwamisha zoezi hilo.
Hata
hivyo,uongozi wa shule pamoja na bodi ya shule hiyo wameishukuru Kampuni ya
Tanga Simenti kwa msaada huo na kusema kuwa ujenzi huo utaondoa changamoto ya
watoto wa kike na kuongeza ufauru katika shule hiyo.
Na
Michael Mgozi.
Comments
Post a Comment