MVUA YA MAWE YAHARIBU ZAIDI YA HEKARI 300 KIJIJI CHA IKANDILO GEITA
Zaidi ya hekari
300 za mazao mbalimbali katika
kijiji cha Ikandilo Kata ya Nyarugusu Mkoani Geita zimeharibiwa na Mvua ya mawe huku wananchi
wa eneo hilo wakihofia kukumbwa na baa la njaa.
Afisa mtendaji wa
kijiji hicho Bw,Furaha Manyanda
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa Mvua hiyo imeharibu mazao mbalimbali
ikiwemo maharage ,Mahindi na Pamba pamoja na baadhi ya nyumba kubomolewa.
Bwn, Manyanda ameeleza kuwa suala hilo limepelekea wakazi
hao kukosa usingizi wakiwaza wataweza kwenda na kasi ya msimu wa
kilimo kwa wakati huu ikiwa msimu wa
kupanda baadhi ya mazao umeshapita.
Hata hivyo afisa mtendaji huyo amewaomba wakulima kuacha kukata tamaa na
badala yake walime mazao yanayostahimili ukame ikiwemo mtama, na mihogo huku akidai kwa wamepanga kuitisha
kikao na wakulima ili kujadilia changamoto hiyo.
Comments
Post a Comment