AFIKIKISHWA MAHAKAMANI KISA UBAKAJI NA KUMPATIA UJAUZITO MWANAFUNZI
Mtu mmoja amefikishwa
katika mahakama ya wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma ya
makosa mawili likiwemo la ubakaji.
Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Monika
Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi inspekta Slyvester Mwaiseje
amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ibrahim Mohamed mwenye umri wa miaka 22
mkazi wa Nyehunge wilayani hapa.
Mwaiseje amesema kuwa mshitakiwa anashitakiwa kwa kosa la kubaka kinyume na kifungu cha 130
kifungu kidogo cha kwanza na cha pili [e] na kifungu cha 131 kidogo cha kwanza
cha kanuni ya adhabu ambapo amembaka
msichana mwenye umri wa miaka 17 ambae jina lake limehifadhiwa anaesoma kidato cha pili wilayani
Sengerema.
Mshitakiwa ametenda kosa hilo Juni
mwaka huu majira ya saa 2 usiku katika kijiji cha
Nyehunge wilayani humo mkoani mwanza.
Kosa la pili ni kumpatia ujauzito msichana huyo kinyume na
kifungu cha 5 cha kanuni ya adhabu ya elimu mwaka 2003 kinachotokana na kifungu
cha 35kidogo cha 3cha sheria ya elimu namba 25 cha mwaka 1978 kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002
Mshitakiwa amekana kosa hilo na amedhaminiwa hivyo kesi hiyo itatajwa tena kwa maelezo ya
awali desemba 27 mwaka huu
mahakamani hapo.
Na, Happyness Paul.
Comments
Post a Comment