MASOMO YA ZIADA YAONGEZA ULEWA WA WANAFUNZI WILAYANI SENGEREMA


Kutokana na umuhimu wa masomo ya ziada kwa wanafunzi, wazazi na walezi  wilayani sengerema wameombwa kuwapeleka wanafunzi kupata masomo hayo wakati huu wa likizo ili wajiendeleze   kimasomo.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu walipo zungumuza  na Radio Sengerema na kusema kuwa ni vyema  wazazi wakawaendeleza kimasomo  wanafunzi  wawapo nyumbani ili kuwajengewa uelewa  zaidi .  
 
Nao baadhi ya wanafunzi    wamesema kuna  umuhimu  mkubwa  kupata    masomo  hayo   ya  ziada wakati wa  likizo  kwani  yatawajenga    kitaaluma.

Sanjari na hayo  walimu hao  wameongeza kuwa   wazazi na walezi  wanajukumu la kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ikiwemo kupitia madaftari   yao   kila watokapo  shuleni ili kujua maendeleo yao.

 Na Ester Mabula.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA