WAZAZI WAHIMIZWA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO WILAYANI SENGEREMA

Wazazi wameombwa kuzingatia  elimu  inayotolewa kuhusiana na  uzazi wa mpango  ili kupunguza ongezeko la watoto wanaoishi maisha duni pamoja  na kulinda afya za akinamama.

Hayo ameyabainisha  Muuguzi Mfawidhi wa  hospital ya  wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza  Bi. Kiaruzi Yegela alipozungumza na Radio Sengerema  ofisini kwake   na kusema kuwa ni vyema wazazi  kuzaa idadi ya watoto wanao weza kuwa hudumia.


Sambamba  na  hayo Bi. Yegela amewasisitiza  hasa akina mama wajawazito   kufika kwenye vituo vya afya ili kufanyiwa  utafiti wa magonjwa  ya moyo pamoja  na maendeleo ya mtoto  alieko tumboni.


Vilevile  Muuguzi huyo  ameongeza kuwa   ni muhimu  wanajamii  kutumia  dawa kwa kufuata  maaelekezo ya wataalamu wa afya.
Na Bwiza Boniphace.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA