MAMA WAJAWAZITO WA KIJIJI CHA NYAMIZEZE WILAYANI SENGEREMA WAONDOKANA NA ADHA YA KUJIFUNGULIA NJE YA ZAHANATI
Akinamama wa
kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema Wameondokana na
tatizo la kujifungulia
njiani kwa muda mrefu kutokana na zahanati hiyo kujenga chumba cha
kujifungulia akinamama.
Hali hiyo imekuja
kufuatia miezi mitano iliyopita Radio Sengerema kuzulu katika zahanati hiyo na
kurusha habari inayohusiana na kero hiyo.
Wakizungumza na Radio
Sengerema baadhi ya akinamama wa kata
hiyo wakionyesha nyuso za furaha
wameishukuru radio sengerema kwa kutumika kama daraja la kuwasaidia
kutatuliwa adha hiyo.
Suzana Busasa
Kazimili ni mmoja wa wauguzi
katika zahanati ya Nyamizeze anakiri
Radio Sengerema imeleta mageuzi makubwa
katika zahanati hiyo kwani imekabiliwa
na ukosefu wa chumba cha kujifungulia kwa muda mrefu.
Mganga Mfawidhi
wa Zahanati hiyo
Bi,Zuhura Ramadhani ameipongeza
Radio Sengerema kwa kurusha habari hiyo na kuleta
mafanyikio.
Radio Sengerema imerusha
habari ya ukosefu wa chumba cha kujifungulia
akinamama katika zahanati ya Nyamizeze Agost 20 mwaka huu na hatimaye imezaa
matunda.
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment