WAHUDUMU WA AFYA WANALAZIMIKIA KUISHI NYUMBA ZA KUPANGA KUTOKANA NA UKOSEFU WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA AFYA NDELEMA GEITA
Baadhi ya watumishi wa zahanati ya
kijiji cha Ndelema kata ya Kamena mkoani Geita wanalazimika kulala
kwenye nyumba za kupanga zilizopo umbali mrefu kutokana na ukosefu wa nyumba za
watumishi katika zahanati hiyo kwa zaidi ya miaka 3.
Akizungumza
na Radio Sengerema Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Bi, Slivia Fabiani amesema kuwa kero hiyo imekuwa ni ya muda mrefu
lakini kwa sasa tayari serikali ya kijiji cha Ndelema na serikali ya mkoa wa
geita wameanza zoezi la kusomba mawe na mchanga ili kuanza ujenzi wa nyumba za
watumishi hao mara moja.
Mbali
na changamoto hiyo Mganga Mfawidhi ametaja kuwa zahanati hiyo inakabiliwa na
upungufu wa watumishi kwani kwa sasa kuna watumishi watatu pekee hali ambayo
inapelekea kufanya kazi bila kupata muda wa kupumzika sambamba na kushindwa
kumudu kuwahudumia wagonjwa kwa wakati.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa upungufu wa
watumishi katika zahanati hiyo huwalazimu kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa
matibabu hali ambayo inapelekea wachelewe kurudi nyumbani.
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment