WAZAZI WATAKIWA KUWAJENGEA MAISHA MAZURI WAKATI WA KUJISOMEA WATOT WAO
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Afisa Elimu shule
za sekondari katika Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza Bwn Godwin Balongo amesema utaratibu wa
wanafunzi kupata chakula shuleni wakati wa masomo unatarajia kurejeshwa tena
mwaka 2018.
Bwana
Balongo amesema awali zoezi hilo lilikwamishwa na mwitikio
hafifu wa wazazi kuchangia chakula cha watoto wao wakiishinikiza kuwa serikali
ya awamu ya tano imeleta neema ya mfumo wa elimu bure hivyo hawakuwa tayari
kuchangia.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa mwaka ujao ni wakati muafaka
kwa wazazi wote kuzingatia agizo hilo ili wanafunzi wasome katika mazingira
rafiki.
Bwna Godwin amedai kuwa
ikiwa wazazi wataunga mkono suala hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Na,BWIZA BONIPHACE
Comments
Post a Comment