WANANCHI WATESWA NA UHABA WA MAJI LICHA YA MAJI YA KISIMA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI KIJIJI CHA NYAMILILO SENGEREMA

Wananchi wa kijiji cha Nyamililo kata ya Kasungamile wilayani Sengerema   mkoani Mwanza  wamelalamikia  mradi mpya wa maji ya kisima kushindwa kutoa huduma hiyo kama ilivyokusudiwa hali inayopelekea  wananchi kuendelea  kukabiliwa na uhaba wa maji.
Image result for PICHA YA  MAJI BUCHOSA

Hayo yamebainishwa na wananchi walipoongea na Radio Sengerema kijijini hapo wameitaka serikali kumaliza tatizo la mradi wa kisima hicho.

Diwani kata ya Kasungamile  Julias Mussa Ndekeja aidha amekiri kuwa toka mradi huo uzinduliwe haujafanya kazi yake ipasavyo hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo linashughulikiwa

Mradi wa  kisima kirefu cha maji cha Nyamililo ni miongoni mwa miradi  iliyozinduliwa katika wilaya ya Sengerema kwenye mbio za mwenge mwaka huu ulitegemewa kumaliza tatizo la uhaba wa  maji kwa wananchi wa kijiji cha  Nyamililo.
Na Charles Sungura

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA