WANANCHI MJINI SENGEREMA WAHIMIZWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Wananchi wilayani Sengerema
Mkoani Mwanza wamehimizwa kuzingatia utunzaji
wa mazingira kwa kupanda
miti hasa katika
msimu huu wa
mvua.
Hayo yamebainishwa na
Afisa maliasili wa Halmashauri ya Sengerema
Bwn Paul Ponsian wakati
akiongea na Redio
Sengerema ofisini kwake,ambapo
ameeleza kuwa kwa
yeyote anaehitaji kibari
cha kukata mti
ni lazima awe
na miti isiyopungua
5 ili kuendelea
kutunza mazingira.
Bwn Ponsian
ameongeza kuwa katika
msimu huu miche
iliyooteshwa ni
milioni mbili na
laki tatu na iliyopandwa
ni miche laki
nane na elfu
sitini, kutoka vitaru mbalimbali ikiwemo vya Nyanchenche,Katungulu,Ibanda,
Chamabanda Bwawani mazingira
na kitaru kilichopo
halmashauri ya Sengerema .
Aidha Afisa huyo
amesema, wana wataalamu wa
mazingira katika maeneo
mbalimbali kwa ajili
ya kuhakikisha elimu
ya upandaji miti
na utunzaji wa
mazingira inawafikia watu
kwa urahisi.
Ameeleza kuwa wameanzisha
mkakati wa upandaji
miti pembezoni mwa Barabara
na kwamba kwa
sasa wamepanda miti
kutoka Bomani hadi
soko la Nyatukara
ambapo malengo yao
ni kupanda miti
katika barabara zote
za wilaya ya
Sengerema.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment