UFAULU WA DARASA LA SABA WAONGOZEKA KWA ASILIMIA 6 WILAYANI SENGEREMA

Kutokana na kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba Kitaifa  wanafunzi Elfu sita mia tisa themanini na nne (6984) wilayani sengerema  mkoani Mwanza wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mwaka  2018.

Akizungumza na Radio Sengerema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Afisa Elimu shule za sekondari wa Halmashauri Sengerema Bw, Godwin Balongo ambapo amebainisha kuwa jumla ya watahiniwa Elfu nane mia nne themanini na tatu(8483) sawa na asilimia 99.2 ikiwa wasichana walikuwa ni Elfu nne mia tatu sabini na sita(4376) na Wavulana walikuwa Elfu nne miamoja na saba (4107) ambapo wanafunzi Elfu sita mia tisa themanini na nne ndiyo wamefaulu kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018.

Aidha amebainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 6 ukilinganishwa na mwaka 2016 ambapo ulikuwa asilimia 76.1 na mwaka huu  asilimia 82.3 ikiwa watahiniwa 37 hawakufanya mtihani wavulana wakiwa 29 na wasichana 34 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, mimba za utoto pamoja na utoro.


Hata hivyo amewataka walimu ambao shule zao zimekuwa na matokeo mabaya kubuni njia mbadala ili kuondoa matokeo hayo ambayo hayaridhishi sambamba na hapo wazazi kuwahimiza watoto kujisomea wawapo majumbani pia kuwaendeleza wale ambao hawakufaulu mtihani katika fani nyingine ikiwa lengo ni kuendana na nchi ya viwanda na uchumi wa kati.   
Na Amina Hassan.                                                                           

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA