PANGA LAMNYANG'ANYA MWENDESHA BODABODA PIKIPIKI YAKE WILAYANI SENGEREMA


Mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda aliyetambulika kwa majina ya  Faida Mathias (18) mkazi wa Tabaruka Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amenusurika kuuwawa baada ya kukatwa na  Silaha    aina ya panga sehemu ya kichwa na watu wasiojulikana.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia decemba 14 mwaka huu ambapo mwendesha bodaboda huyo alikodiwa na mtu ambaye hamfahamu baada ya kufika kwenye Nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Sengerema ndipo amemuamuru asimame na ghafula wametokea watu na kuanza kumshambulia  baada ya hapo wamechukua pikipiki yake nayo kutoweka kusikojulikana.


Radio Sengerema imefika hosptali teule ya wilaya ya Sengerema na kuzungumza na Manusura wa tukio hilo   na kusimulia jinsi tukio lilivyo tokea.

Nae mkuu wa kitengo cha usalama barabara wilaya ya Sengerema Inspecta Hamis Wembo amefika  sehemu ya tukio na kuahidi kuitisha kikao mara moja cha waendesha bodaboda kwa ajili ya kuweka mikakati ya kutokomeza matukio hayo.


Matukio ya waendesha bodaboda kutekwa kisha kuchukuliwa pikipiki zao yamezidi kusika kasi katika mji wa Sengerema kwani tukio hili ni tukio la pili kuripotiwa  kutokea ndani ya mwenzi huu.

Na Said Mahera.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA