WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA MIUNDO MBINU YA BARABARA KIJIJI CHA KASUNGAMILE WILAYANI SENGEREMA
Wananchi wa kata ya Kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa
kulinda na kutunza miradi ya
maendeleo wakati serikali inapokamilisha
ujenzi wa miradi hiyo ili iweze kudumu
kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa na
diwani wa kata ya Kasungamile Mheshimiwa Julias Mussa Ndekeja kwenye mkutano wa
wananchi katika kijiji cha Nyamililo alipokuwa akikabidhi mradi wa ujenzi wa
barabara ya Nyamililo kwenda Bulunga baada ya Halmashauri ya Sengerema kukamilisha ujenzi barabara hiyo.
Wananchi wamekuwa na
kilio cha muda mrefu cha barabara ya Nyamililo kwenda Bulunga hivyo imeelezwa kukamilika kwa ujenzi wake kumepelekea wananchi kuipongeza serikali kwa juhudi za
kuwapatia maendeleo na kuahidi kuendelea
kuiunga mkono.
Na Charles Sungura.
Comments
Post a Comment