SHULE YA SEKONDARI YAAHIRISHWA KUFUNGULIWA MWAKA 2018
Wananchi wa kata ya Ibisabageni Wilayani
Sengerema Mkoani Mwanza
wameshangazwa na kitendo cha Serikali kutowapanga
wanafunzi wa kidato
cha kwanza katika shule hiyo
licha ya kukamilika kwa madarasa
ya kidato hicho mwaka huu.
Hayo yameelezwa na wananchi kwenye kikao cha Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Sengerema
CCM Bwn Mark Augustne Makoye ambapo wananchi wamesema kufunguliwa kwa
shule hiyo kutapunguza adha ya wanafunzi kutembea
umbali mrefu kufuata elimu shule za kata jirani.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Bwn Jumanne Masunga
ameshangazwa shule hiyo kutopangiwa
wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu licha ya kuwepo kwa madarasa na kwamba
walitarajia mwaka 2018 itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza rasmi.
Akitolea ufafanuzi
kuhusu kutofunguliwa kwa shule hiyo Afisa Mtendaji wa kata ya Ibisabageni bwn Adam Salum amesema tatizo ni kwamba
haijakamilika kwa maabala na kuiomba
serikali isaidie katika vifaa vya maabala.
Ziara ya Mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi CCM Bwn Mark Augustine Makoye ametembelea kata mbili kata ya Ibisabageni na Nyatukala kwa lengo la
kukagua shuguli za maendeleo.
Na Said Mahera.
Comments
Post a Comment