KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO SHULENI NI MSINGI WA UFAULU MZURI
Walimu wa shule ya
msingi Nyamililo kata ya
Kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza
wamewataka wazazi kufuatilia
maendeleo ya watoto shuleni
ili kujua maendeleo
ya masomo ya watoto
wao .
Hayo yamebainishwa na walimu hao
kwenye kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo walimu wamesisitiza ushirikiano kati ya wazazi na
walimu katika kuinua kiwango cha elimu
kwa wanafunzi.
Pamoja na Serikali ya
awamu ya tano kutoa elimu bure nchini lakini
wazazi wametakiwa kutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha mtoto anaenda
shule ikiwa ni pamoja kumnunulia sare na vifaa vyote vinavyohitajika.
Naye Mwalimu Mkuu wa
shule ya msingi Nyamililo Dominic
Jile amesema kitaaluma shule imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali.
Kwa upande wao
Wazazi wamepongeza kwa mshikamano uliopo kati ya uongozi wa shule na
wa serikali ya kijiji hali iliyopelekea
kufanikiwa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na
kutatua changamoto mbalimbali
shuleni hapo.
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment