SIMU ZATAJWA CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI WILAYANI SENGEREMA
Baadhi ya wazazi na
walezi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamekemea vikali suala la watoto
kumiliki simu wakiwa bado masomoni hususani kwa watoto wa kike ili kuepuka
janga la mimba za utotoni .
Wakiongea na radio
Sengerema kwa nyakati tofauti wamesema kuwa simu ni chanzo kikubwa cha
maadili kumomonyoka kwa watoto.
Hata hivyo wameongeza
kwa kusema kuwa wazazi na walezi wasiwe chanzo cha kupelekea watoto wao
kumiliki simu kwani malezi bora yanatoka kwa mzazi na yanahitaji umakini zaidi.
Pia wazazi wamewasihi
watoto kuzingatia zaidi masomo
ili waweze kutimiza ndoto zao
katika maisha na wawe na utii na nidhamu
kwa wazazi ,walezi na walimu.
Na Glorius Balele.
Comments
Post a Comment