SERIKALI YAANZA KUPELEKA WAHUDUMU WA AFYA KATIKA ZAHANATI YA KISHINDA WILAYANI SENGEREMA
Kutokana na Radio
sengerema kurusha habari ya ukosefu wa
wa hudumu wa afya katika zahanati ya kijiji cha Kishinda kata
ya Kishinda hatimae serikali imeanza kupeleka wahudumu wa afya katika zahanati
hiyo.
Wakizungumza na Radio
sengerema baadhi ya wananchi wa
kijiji hicho wameipongeza radio sengerema kwajitihada
walizozifanya katika kuripoti habari iliyopelekea serikali kuchukua hatua.
Nae mwenyekiti wa
kijiji cha Kishinda MASUMBUKO KAKINDA
ameishukuru Radio sengerema kwakurusha habari zenye tija katika jamii.
Kwa upande wake mmoja
kati ya Wauguzi wa kituo hicho BARAKA JACOBO pia ameishukuru Radio sengerema kwakuibua changamoto katika jamii.
Radio sengerema
imerusha habari ya upungufu wa
wahudumu wa afya katika zahanati hiyo
Apiril mwaka huu ambapo hadi
kufikia desemba mwaka huu tayari serikali imechukua hatua za makusudi
na kuanza kupeleka wauguzi katika
zahanati hiyo.
Na Deborah Maisa.
Comments
Post a Comment