MAMA WAJAWAZITO WATAKIWA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI ILI WAMNUSURU MTOTO ALIYEPO TUMBONI
Akinamama wajawazito
wanatakiwa kuacha kutumia dawa za
kienyeji pindi wawapo wajawazito ili kumnusuru
mtoto aliyepo tumboni.
Hayo ameyabainisha Muuguzi
Mfawidhi wa hospital ya segerema Bi Kiaruzi Yegera amewataka akinamama
wajawazito kuhudhuria klinik ili kuachana
na matumizi ya dawa za kienyeji pamoja na ushauri mbalimbali.
Pia Bi. Kiaruzi
amewataka akinamama wote wakiwemo watumishi wa umma na watumishi
wa sekta binafisi kuzingatia lishe stahiki ili kulinda
afya ya mtoto.
Hata hivyo, Muuguzi
huyo amewasisitiza mama wajawazito wote kufika katika katika vituo
vya afya ili kupatiwa elimu
sahihi kuhusu madhara ya matumizi ya
dawa za kienyeji.
Na,BWIZA BONIPHACE
Comments
Post a Comment