BIA YASABABISHA DEREVA BODABODA KUACHA PIKIPIKI YAKE WILAYANI SENGEREMA.
Dereva pikipiki maarufu
kama Bodaboda amejeruhiwa
na kitu
chenye ncha
kali sehemu za mwili
wake na kisha kutelekezwa pikipiki
yake katika mtaa wa Kanyamwanza kata ya
Mwabaluhi wilayani Sengerema.
Tukio hilo
limetokea usiku wa
kuamukia Desemba 08 mwaka huu
katika mtaa wa kanyamwanza wilayani
Sengerema.
Kwa upande
wake kamanda wa
jeshi la sungusungu
katika mtaa wa huo
bwn, SIMONI MPUYA, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo
na kusema kuwa dereva
pikipiki huyo ni wa kituo cha pikipiki cha Nyanchenche
Road Wilayani humo.
Kamanda Mpuya
amewataka waendesha bodaboda
kuwa makini na
wateja wao wanaowabeba
hasa katika
nyakati za usiku
ili kuepukana na matukio kama
hayo.
Nao baadhi ya
madereva pikipiki
wa mtaa wa Kanyamwanza wamesema
kuwa hali ya
matukio ya wizi
wa pikipiki katika
mtaa huo kwa sasa limekuwa
ni tatizo la muda mrefu
bila kupatiwa ufumbuzi.
Pamoja na na
hayo kamanda Mpuya
amesema katika kuelekea msimu
wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya wamejipanga
vizuri kukabiliana na uhalifu
katika eneo hilo.
Na,Enosy Mashiba
Comments
Post a Comment