BODABODA WATAKIWA KUEPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA SENGEREMA
Madereva pikipiki
maarufu bodaboda wilayani Sengerema wametakiwa kuepuka matumizi ya dawa za
kulevya ikiwemo ulevi na kuzingatia elimu wanayopewa na viongozi wa usalama
barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Mwanza ,kamishina msaidizi wa jeshi la
polisi Tanzania Mkadam Hamiss Mkadam ,alipokuwa akizungumza na umoja wa
waendesha bodaboda wilayani Sengerema mkoani Mwanza na kudai kuwa ni vyema
wazingatie maelekezo yote pamoja na sheria za usalama barabarani
Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Tanzania Mkadam Hamisi Mkadam |
Kwa upande
wao waendesha bodaboda wamesema kuwa watatekeleza na kusimamia sheria za usalama
barabarani kwa umakini ,ikiwa ni pamoja na kupambana na suala zima la matumizi
ya dawa za kulevya.
Sambamba
na hayo kamishina msaidizi wa jeshi la
polisi Tanzania Mkadam Hamiss amesisitiza kuwa ni vyema madereva kuzingatia
usafi kwa hali ya juu ili kulinda afya zao pamoja na abiria .
Na Glorius Balele.
Comments
Post a Comment