KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

Wakazi wa kisiwa cha Zilagula kilichopo katika kata ya Bulyaheke halmashauri ya Buchosa  wilayani Sengerema  wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu hususani katika msimu huu wa mvua zinazo endelea kunyesha.


Wakizungumza na Radio Sengerema katika kisiwa hicho wamesema mazingira wanayoishi siyo salama kwa afya zao kutokana baadhi ya wakazi  wa eneo hilo kutokuwa na vyoo pamoja Nguruwe kuishi pembezoni mwa ziwa hali ambayo mvua zikinyesha uchafu wote hutiririshwa ziwani.
                                                                         
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji katika kisiwa hicho Abushilu Yasini amesema hali ya mazingira ni mbaya hivyo serikali ione umhimu wa kukabiliana na tatizo hilo.

Hata hivyo baada ya jitihada za kuzungumza na Bwana Afya huyo kuwa za kukatisha tamaa, Radio Sengerema ikalazimika kumtafuta  mkurugenzi  wa halimashauri ya Buchosa Bwn, Crispin Luanda kwa njia ya simu na simu iliita bila mafanikio na Radio Sengerema inaendelea kumtafuta ilikujua hatua zipi zinachukuliwa dhidi ya wachafuzi  wa mazingira katika kisiwa hicho.
Licha ya serikali kuzifungia baadhi ya kambi  za Uvuvi na Nyumba za kulala wageni baada ya kubainika nyoo vyake kutirilisha maji taka ndani ya ziwa Victoria,Radio Sengerema imeshudia baadhi ya kambi hizo kuendelea na kutumika huku nyumba za wageni zikibadili mifumo badala wateja kulala sasa zimekuwa zikitoa huduma ya choo kwa kutoza fedha,huku baadhi ya makanisa  yakiwa hayana vyoo hali ambayo waumini  hupata shida  pale wanapo hitaji huduma hiyo.
Kisiwa cha zilagula ni miongoni mwa visiwa vilivyopo katika Halmashauri ya Buchosa,kinacho  kadiliwa kuwa na watu 2000 hadi 4000  na mwaka 2015  ugonjwa wa kipindu pundi umetajwa wakumba wakazi wa kisiwa hicho na watu kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo

Na Katemi Lenatus.


Comments

  1. Napakumbuka sana zilagula nimepamis sana

    ReplyDelete
  2. Jaman nilitaka kujua saizi debe la dagaa ni shingapi huko zilagula

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA