Posts

Showing posts from September, 2017
Image
MABOMBA YAPO ILA MAJI HAYATOKI TUNATESEKA MNO"WANANCHI" Wakazi wa mjini Sengerema mkoa wa Mwanza wameilalamikia idara ya maji kwa kukosa maji wiki ya pili sasa na hawajui tatizo nini hali ambayo imewalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama kwa matumizi ya binadamu . Wananchi hao wamesema hawajui tatizo hilo litachukua muda gani kwani mpaka sasa wanapata usumbufu mkubwa kupata huduma hiyo muhimu. Kufuatia hali hiyo Radio Sengerema imemtafuta Meneja wa maji Mjini  Sengerema Eng,Christopher Kiwone amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa mpaka sasa wanalifanyia kazi hivyo muda sio mrefu huduma hiyo itarejeshwa. Aidha wananchi wameitaka mamlaka husika kulitatua tatizo haraka iwezekanavyo kwani imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi mjini Sengerema wanaotumia maji ya bomba. Na Deborah Maisa    
Image
UVUVI HARAMU WAGEUKA KAA LA MOTO KUTOKOMEZWA Nyavu haramu zikiteketezwa kwa moto Juhudi za kupambana na uvuvi haramu zimeonekana kutozaa matunda katika ziwa victoria wilayani sengerema mkoani mwanza na hivyo kutishia ustawi wa halmashauri ya buchosa ambayo zaidi ya asilimia 80 ya mapato yake ya ndani yanatokana na sekta ya uvuvi. Wakizungumza  wakati wa kikao cha dharura cha baraza la madiwani la halmashauri ya buchosa,baadhi ya madiwani wamewanyoshea vidole wataalam waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya uvuvi kwa kuwa ni kikwazo kwenye kutokomeza uvuvi haramu. Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru ) wa wilaya ya sengerema Bwn, Protas Sambagi amekiri kutofanikiwa kwa juhudi za kukomesha uvuvi haramu huku akitaja sababu kubwa kuwa rushwa. Akizungumzia hali hiyo,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Buchosa Bwn, Crispian Luanda   amesema kuwa hatua zimeanza kuchukuliwa kwa baadhi ya wataalam wa uvuvi wanaonyoshewa vidole. Kikao cha dharur
Image
UKOSEFU WA HUDUMA ZA AFYA ZAWATESA WANANCHI ZAHANATI Wananchi  wa  kijiji  cha  Butonga   kata  ya  Igulumuki  wilayani  Sengerema  wamelazimika  kutembea  umbali    mrefu  ili kupata  huduma  za matibabu Kutokana na ukosefu wa zahanati katika kijiji hicho  . Hayo  yamebainishwa  na mwenyekiti  wa  kijiji  hicho bwana  Thobias  Shija  Isangu wakati  akizungumza  na Radio  Sengerema  na kusema kuwa hali  ya  huduma ya  afya sio  rafiki kwani wananchi  hao  wanalazimika  kutembea  umbali  mrefu ,kufuata huduma za afya katika   zahanati  ya kijiji jirani cha  Igulumuki ambapo   hali  hiyo inapelekea  kuhatarisha  maisha  yao. Hata  hivyo    Bwana  Isangu    ameongeza  kuwa  kwa sasa  wanamajengo ya   zahanati  lakini  wanahitaji  msaada wa  kutosha ili waweze  kukamilisha  ujenzi  wa zahanati  hiyo na kuondokana na adha inayowakibili kwa muda mrefu sasa. Na Enosy Mashiba
ULINZI WAIMARISHWA Kutokana na wizi wa mali za wananchi uliokuwa umeshamili kwa kasi hapo awali  katika kijiji  cha  Butonga    wilayani Sengerema   kwa sasa  wameendelea  kuukomesha   kwa  kushirikiana  na jeshi  la Jadi  maarufu kama sungusungu. Hayo  yamebainishwa  na mwenyekiti wa kijiji hicho,Bwn Thobias Shija Isangu   ambapo amesema kuwa   kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanaishi kwa kuhofia usalama wa mali zao na kuongeza   kuwa   kwa sasa hali ni shwari. Aidha  mwenyekiti  huyo  ameongeza  kuwa  kwa  sasa  wamekaa  na  jeshi  la  jadi  sungusungu  pamoja  na wananchi  katika  kuimarisha  ulinzi  na  usalama  katika  kijiji  hicho. Bwn Isangu amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa  na kuwataka waendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili waweze kutokomeza suala hilo. NA MICHAEL MGOZI.  
Image
KULIPA MADENI WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA Zao la Pamba Wakulima wa zao la pamba wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kulipa madeni yao wanayodaiwa ili kusaidia upatikanaji wa pembejeo msimu huu wa kilimo mwaka 2017/2018. Akizungumza na Radio Sengerema Afisa kilimo Ushirika na umwagiriaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Bwn;Simon Butera amesema ni vyema wakulima wote waliochukua pembejeo za zao la pamba msimu uliopita kulipa madeni yote mapema ili kujiandaa na msimu huu mpya wa kilimo. Kwa upande wake Afisa ugani wa kata ya Igalula wilayani hapa Bwn,Stanley Shija kupitia kikao cha diwani wa kata hiyo amesema katika kijiji cha Nyasigu amewaasa wakulima wa zao hilo kulipa madeni hayo. Aidha  wakulima wote wametakiwa kuanza kuandaa mashamba yao kwa kukatakata  masalia ya  zao hilo mashambani Na Elisha Magege
Image
MAHAKAMANI KISA NYAVU HARAMU Watu watatu wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kupatikana na nyavu haramu.  Akisoma shitaka linalowakabili mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bi,Subira Mashambo mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspecta Sylvesta Mwaiseje amewataja watuhumiwa kuwa ni Edwin Michael  mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mkolani Mwanza Ernest Manyecha (62) mkazi wa Ukiliguru Misungwi na Fitina Juma (65) mkazi wa Mkomba Busisi. Inspecta Mwaiseje amesema kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la kupatikana na nyavu haramu kinyume na kifungu namba 66 kifungu kidogo cha kwanza A na kifungu kidogo cha 4 cha kanuni ya uvuvi kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa mnamo septemba 23 mwaka huu majira ya 07:00 mchana huko katika maeneo ya Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwa pamoja walipatikana na nyavu haramu moja aina ya kokoro kinyume cha sheria. Hata hivyo washitakiwa wote kwa pamoja wamekan
Image
SUNGUSUNGU LAWACHAPA    VIBOKO WANANCHI Viongozi wa Jeshi la Jadi wakiwa na Msaidizi wa  sheria wilayani sengerema James Sendama (wa pili kutoka kushoto) Baadhi ya wananchi   wa   kijiji  cha   Bungonya    kata  ya Nyamazugo   Wilayani  Sengerema       wamelilalamikia  Jeshi   la    jadi    maarufu  kama    Sungusungu  la   kijiji  hicho  kwa   kuwachapa  viboko  na kuwatishia  kuwafukuza  katika   eneo  hilo  bila  kosa lolote.          Baadhi ya wananchi ambao ndungu zao wamekumbwa na tukio hilo la kuchapwa  viboko  wamesikitishwa na kitendo cha jeshi la jadi  kwa maamuzi  yake     kwa  kuwa  moja ya jukumu la jeshi la jadi  ni kuwakamata wahalifu na kuwafikisha  kwenye vyombo vya  dola   ili wachukuliwe  hatua na  siyo   kuwachapa   ovyo   viboko.       Wajumbe  wa  serikali  ya kijiji hicho wamesema kutokana na sakata hilo viongozi wa kijiji cha Bungonya wanatakiwa  kuwafundisha  viongozi wa jeshi la jadi mipaka ya kazi yao ili kuepuka  kujitia   matatani. Nae
Image
WAKULIMA CHANGAMKIENI KILIMO MSIMU HUU WA MVUA "Diwani Ndekeja" wakulima Wananchi  kata ya Kasungamile  wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa  kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kilimo na kuacha kukaa vijiweni muda kufanya kazi. Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Kasungamile Mh;Julias Ndekeja alipozungumza na redio Sengerema ofisini Diwani Ndekeja amesema pamoja na kulima mazao ya chakula ameshauri na kuwahamasisha wananchi kulima zao la pamba  kama zao  la biashara ili kuongeza kipato. Aidha Ndekeja amewataka wakulima kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo  walio kwenye kata zao ili kulima kilimo chenye tija wakati serikali inaendelea kutatua changamoto ya pembejeo.  Na Charles Sungura.
Image
 MBWA ASABABISHA KIFO SENGEREMA. Mbwa picha ya mtandao Mtoto  mmoja amefariki dunia baada ya kung’atwa na mbwa katika kijiji cha Ibondo kata ya Ibondo Wilaya Sengerema mkoani mwanza. Mtoto huyo amefahamika kwa  majina ALPHONCE SIKITU (8) aliyekuwa akisoma darasa la kwanza shule ya msingi Ibondo  kata ya Ibondo  wilayani  hapa.   Akisimulia kisa hicho bibi wa mtoto huyo Bi   Helena Shubalu       ameeleza kilichotokea mpaka    kupelekea mtoto alphonce   kupoteza maisha. Kwa upande wake mkuu wa shule ya Ibondo alipokuwa  akisoma mtoto huyo Mwl   Emmanueli Mashili amesikitishwa na kifo cha  mtoto huyo kwani alikuwa akihudhuria darasani kama kawaida licha ya kuwa hakupewa taarifa ya kung’atwa na mbwa. Naye diwani wa kata hiyo Mathias Mashauri amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wamiliki wa mbwa kuhakikisha wanawachanja mbwa wao chanjo ya kuondoa sumu mwilini. Matukio ya watu kung’atwa na mbwa yamekuwa yakiendelea kutokea na hili ni tukio la
Image
MKUU WA MKOA WA ARUSHA LEO ANAANZA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa waArusha Mrisho Gambo leo anaanza Ziara yake ya   siku moja kutembelea  vijiji kwa lengo la kujibu kero zilizoibuliwa na wananchi mbele ya Rais Magufuli.
Image
AFISA MTENDAJI ATUHUMIWA KUTAFUNA PESA ZA WANANCHI Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyangh’wale kata ya Nyanghwale mkoani Geita bw, Ramadhani Masele Manyero anatuhumiwa  kutafuna pesa za wananchi  sh. Milioni moja zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya ukarabati wa lambo la maji liloharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwaka jana. Mbele ya kikao cha wananchi kilichohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale bw, Hamim Gwiyama na mbunge wa jimbo hilo bw, Hussein Nassoro ambacho kililenga kutathimini jumla ya fedha zilizochangwa na wananchi pamoja na utekelezaji wake. Nae Afisa Mtendaji anaetuhumiwa kutafuna pesa za wananchi bw,Ramadhani Nasoro  Manyero amekana mbele ya mkuu wa wilaya hiyo kutumia pesa hizo za wananchi ambazo zilichangwa shilingi 6500 kwa kila kaya. Hata hivyo mkuu wa wilaya bw, Hamim Gwiyama amemtaka Afisa mtendaji huyo kufika kituo cha polis kilichopo Karuma mapema akiwa na mchanganuo sahihi juu ya matumizi ya pesa hizo baada ya kutoridhishwa  na
Image
KILABELA YAIMALISHA ULINZI SILAHA Balozi  wa  mtaa wa  Kilabera B , kata ya Nyatukala wilayani  Sengerema  mkoani  Mwanza Bi, SPESIOZER  PAUL   amesema  wanaendelea kushirikiana    na Jeshi la  polisi ili  kuimarisha ulinzi  katika  eneo  hilo. Balozi  huyo amesema hayo  wakati  akizungumza  na Radio  Sengerema  na  kusema  kuwa hali  ya  usalama katika  mtaa  huo  ni  shwari  kutokana  na  juhudi  wanazozifanya  za  kushirikiana  na jeshi la polisi na kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano. Pia  balozi  huyo  ameeongeza  kuwa wanahitaji  ulinzi  shirikishi  ili  kuzuia uharibifu wa  aina  yoyote  katika  eneo  hilo  na  hata  maeneo  mengine  kwa  ujumla. Aidha  bi,  Spesiozer   amewaasa  wazazi na  walezi  kutambulisha  wageni  wao  wanaokuja  katika  eneo  hilo  ili  kuepukana  na mwingiliano wa watu  mbalimbali kwani  itawasaidia  kuwabaini watu  wanaoingia  bila  kufuata utaratibu  wa  mtaa  huo. Na Enosy Mashiba
Image
MTO WASABABISHA WANAFUNZI KUSHINDWA KWENDA SHULE MTO Wanafunzi  100 washindwa kuhudhuria masomo katika  shule  ya sekondari ya Kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza kutokana  na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mto kufurika maji.   Kutokana na kuwepo Kwa adha hiyo Redio Sengerema imemtafuta  diwani kata ya Kasungamile Mh   Julias Ndekeja ili kujua amejipangaje kutatua kero hiyo iliyosababisha wanafunzi kushindwa kuhudhulia masomao. Wananchi pamoja na Wanafunzi wa kijiji cha Nyamililo  hushindwa kupata huduma muhimu za matibabu, elimu na utawala wakati wa  masika kutokana na mto huo kufurika hivyo wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu ili  waondokane na adha hiyo . Na Charles Sungura
Image
WAKULIMA WAPATIWA PEMBEJEO ZA KILIMO Mkulima Wakulima wa zao  la pamba  Wilayani Sengerema  wametakiwa  kuendelea  kujiandikisha  ili kupatiwa pembejeo za kilimo       kwa kuwa  zoezi  hilo  bado  linaendelea  katika vijiji vyote kwa wakulima wa zao hilo.    Akizungumza na Radio Sengerema Afisa kilimo Ushirika na Umwagiliaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Bwn,Simon Butera amesema zeozi hilo linaendelea kwa wakulima wote wa zao hilo. Akielezea hasara za wakulima hao kutojiandikisha amesema hawata pata pembejeo za  kilimo    kama vile mbegu na dawa za kupulizia wadudu. Hivi   karibuni   Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi ambae pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa Dkt;Charles Tizeba  katika ziara yake ya  kuwashukuru wananchi wa jimbo lake amesisisitiza  jambo  hilo la kujiandiisha  huku   akiwataka  wananchi kuwa  na  tabia  ya  kutunza  mazao. Aidha Bwn;Butera  amesema   zoezi hilo linafanywa chini ya usimamizi wa mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh, Emmanuel Kipole hi
Image
Rais Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422. Rais Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, leo amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo mbali mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha. Tukio hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjni, limehudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa na mafisa wa Jeshi nchini pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha. Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli amekagua gwaride maalum, na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao. Tukio hilo la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  ni la kwanza kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.
Image
Kamati za  shule simamieni mahudhurio ya wanafunzi “Aron Laiza” wanafunzi Halmashauri ya wilaya ya Sengerema imesema haitasita kuwachukulia hatua wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule. Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya ya Sengerema BWN ARON LAIZA kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Sengerema katika Hafla ya wiki ya elimu ya watu wazima ambayo yamefanika katika shule ya msingi Ibondo wilayani Sengerema. Amesema kamati za shule zisimamie mahudhurio ya wanafunzi na endapo mzazi atabainika kukwamisha maendeleo ya mwananfunzi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kupelekwa mahakamani. Kwa upande wake Kaimu Afisa elimu ya watu wazima wilaya ya Sengerema  Bwn Deogratius F Munema amesema katika elimu ya watu wazima kunachangamoto nyingi zinazo pelekea kushindwa kufikia malengo waliojiwekea Hata hivyo maadhimisho hayo yamefikia kilele ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kisomo katika ulimwengu wa sayansi na teknolijia kwa maendeleo ya nchi Deborah Maisa. 
Image
Pongezi kwa rais Magufuli Rais Dkt John Pombe Magufuli Mchunganji wa kanisa la AGAPE lililopo Shinyanga Mch, Moses Maduhu ameipongeza serikali ya  muungano    wa  Tanzania ikiongozwa na Rais John Pombe Magufuri   kuboresha elimu nchi kwa kuhakikisha inawapa kipaumbele watoto wa kike ili kufikia malengo yake.. Hayo ameyaeleza kwenye mahafari ya tatu ya darasa la saba katika shule ya mchepuo wa kiingereza Sayuni na kudai kuwa  serikali ya awamu ya tano  imezidi kutatua changamoto hususani katika sekta ya elimu. Pia amewaomba wahitimu hao kuepuka vikwazo ambavyo watakutanavyo kwani vitawafanya kutotimiza malengo yao pia nao wazazi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa watoto. Awali akijibu lisala iliyosomwa na G oodluck James    ambayo shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali licha ya kuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mithiani ya kuhitimu. Nao wahitimu  wamesema watahakikisha wanazingatia ushauri wa mgeni rasmi. Mchungaji Mose Maduhu ameahidi kutatua changam
Image
SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUMALIZA KERO YA MAJI SAFI NA SALAMA waziri wa Tanzania Kassim Majaliwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma. Amesema serikali kupitia kampeni ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati  akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema, Bicha na Bereko akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi. Waziri Kassimu amesema kwa sasa Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu, vifupi pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya hiz
Image
UDHALILISHAJI WAMFIKISHA MAHAKAMANI Mtu  mmoja  amefikishwa  katika  mahakama   ya   wilaya   ya  sengerema  mkoani  mwanza  kwa  tuhuma   ya  udhalilishaji. Akisoma  shitaka   linalomkabili   mbele   ya   hakimu   wa  mahakama  hiyo  Bi  Monica   Ndyekobora   ,Mwendesha  mashitaka  wa  jeshi   la  polisi  INSPECTA  SLIVESTA  MWAISEJE,amemtaja   mshitakiwa   kuwa  ni  MWITA   TULETWA  mwenye   umri  wa   miaka  18   mkazi  wa Nkome   Geita.  INSPECTA    MWAISEJE  amesema   kuwa  mshitakiwa  anashitakiwa   kwa   kosa  la  udhalilishaji  kinyume   na   kifungu  namba  135   cha   kanuni   ya  adhabu   sura   ya   16,  kuwa  mshitakiwa  MWITA   TULETWA   anashitakiwa  mnamo  septemba  11   mwaka   huu   majira   ya   saa  10:00   jioni  huko  katika  kisiwa  cha  Zilagula   wilayani  Sengerema  mkoani   Mwanza  kwa   makusudi  na   isivyo   halali  kumshika msichana ambaye   jina  lake  limehifadhiwa  sehemu za mwili wake bila  lidhaa   yake. Hata    hivyo   mshitakiwa   ameka
Image
Rais Magufuli awasili Jijini Arusha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,John Pombe Magufuli leo amewasili mkoani Arusha kuanza ziara yake ya kikazi ya siku 3 mkoani Arusha pamoja na Manyara. Kwenye ziara hiyo Rais Magufuli atafungua barabara ya lami  kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Baada ya uzinduzi huo atazungumza na wananchi na baadaye kurejea Arusha, ambapo anatarajiwa kutoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi.
Image
MFUMO UPIMAJI WA VIWANJA WAZINDULIWA KIWANJA Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa kushirikiana na kampuni ya Amboni Land Consalt imeamua kuanzisha mfumo wa upimaji wa viwanja kwa lengo la  kuwaelimisha wananchi pamoja na kutumia mfumo wa hati miliki na namba za kudumu za viwanja. Akitoa elimu hiyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw,Rweikiza katika kikao kilichofanyika katika kata ya  Ibisabageni wilayani  Sengerema, amewataka  wananchi kutokuwa na shaka juu ya mfumo huo kwa kusema kuwa upimaji huo hauhusiki na kubomolewa kwa nyumba zao. Nae Mwenyekiti  wa Mtaa wa Ibisabageni Bw,Henry Kakele  amewaomba wananchi kuwa na subira na kuwahakikishia kwamba ombi   lao litafika panapo husika. Hatahivyo Mwenyekiti amehitimisha kikao kwa kuwaomba wananchi wote  mitaa yote miwili Busisi Road na Ibisabageni,kuteuwa wajumbe wawili kila mtaa watakaounda kamati ya upimaji huo. Na THOBIAS NGUBILA
Image
AGIZO BODABODA  piki piki(Boda boda) Waendesha pikipiki  Maarufu kama bodaboda wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kubeba  watoto walio chini ya umri wa miaka tisa  kwa kuwa ni makosa  kwani   watoto hao hawamudu kusafirishwa wakiwa peke yao bila uangalizi wowote.     Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki wilayani Sengerema    Bwn,Joseph Emmanuel Augustine katika mahojiano na Radio Sengerema ambapo amesema hii ni sheria ya nchi na ni kosa kubwa kubeba mtoto kwenye pikipiki bila kuwepo  mwangalizi. Katika hatua nyingine Bwn,Augustine amesema ni vyema jamii nzima kutoa ushirikiano wa kutoa elimu ,na kuwaomba wandesha pikipiki kufuata sheria kwani vitu vingi wamepitia ikiwemo sheria ya kuwa na kofia mbili ngumu.   Na Elisha Magege.  
Image
NYAVU HARAMU ZAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU 3. nyavu haramu za uvuvi Watu  watatu   wamefikishwa   katika  mahakama   ya  wilaya  ya  sengerema   mkoani  mwanza   kwa   tuhuma  ya   kupatikana  na  nyavu  haramu  aina  ya  timba. Akisoma  shitaka  linalowakabili  mbele  ya   hakimu   wa  mahakama  hiyo  BI  MONIKA  NDYEKOBORA ,mwendesha  mashitaka  wa  jeshi  la  polisi  INSPECTA  SLIVESTA  MWAISEJE  ,amewataja  washitakiwa  kuwa  ni  MASUMBUKO  GEREVASI  mwenye  umri  wa  miaka  45  dereva, OMARY   TWENTIY  mwenye  umri  wa  miaka  67, na  RAMADHANI  ISSA  mwenye  umri  wa  miaka  25  Wote   ni   wakazi   wa   kijiji   cha  Nyakarilo  wilayani  Sengerema. INSPECTA   MWAISEJE   amesema   kuwa  washitakiwa  wanashitakiwa   kwa  kosa  la  kupatikana  na  nyavu   haramu   kinyume   na  kifungu  namba  66   kifungu  kidogo   cha   (1)  A  na  kifungu  kidogo   cha   4    cha   kanuni   za   uvuvi  ya  mwaka   2009   kinachotokana  na  kifungu  namba   57  cha   sheria   ya  u
Image
WAKULIMA WILAYANI MISUNGWI WAPEWA MAFUNZO YA KUTUMIA HATI MILIKI. Jembe Wakulima wa kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi mkoani Mwanza wamepewa mafunzo ya namna kutumia hati miliki za mashamba za  kimila kwa lengo la kuchukulia mikopo ili kujiendeleza kimaisha. Akizungumzia lengo la mafunzo hayo meneja wa Mulabika ambao ndiyo wanaotoa mafunzo hayo Makame Juma amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wakulima hao kujikwamua kimaisha kwa kupata mikopo kwa kutumia hati hizo. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi Fredrick Nyoka amesema kuwa kati ya vijiji 113 katika wilaya hiyo ni vijiji viwili ambavyo vilichaguliwa katika mpango huo ambayo ni Kasololo na Matare Mnamo mwaka  2012. Nao baadhi ya wakulima waliohudhuria  katika mafunzo hayo wameshukuru kuanzishwa kwa mpango huo na kwamba utawasaidia kujikwamua kimaisha. Na Veronica Martine.
Image
WATAKAOPANDA MAZAO MAREFU NDANI YA MAMLAKA YA MJI WA SENGEREMA FAINI YA SHILINGI LAKI MBILI MAZAO YA MAHINDI Mwenyekiti    wa    Mamlaka   ya     Mji     Mdogo    Mjini Sengerema     Bwn Richand Buluma amewatangazia kiama watu ambao watapanda mazao marefu ndani ya mamlaka ya  mji wa Sengerema msimu huu wa kilimo. Hayo ameyasema wakati akiongea na Radio Sengerema mapema hii leo bwn Buluma amewataka wananchi kutokujihusisha na kilimo hicho katika maeneo ya mjini. Hata hivyo Bwn Buluma ameeleza kuwa watakaokiuka  agizo hilo  watatozwa faini ya shilingi laki mbili 200,000 akishindwa kulipa faini hiyo atafikishwa mahakamani na atafungwa miezi 6 jela. Kufuatia tamko hilo Diwani wa kata ya Nyatukala Mh Salleh Msabaah amewaomba wananchi wake kuachana na kulima mazao marefu katika maeneo yao kwani ni kinyume cha  sheria. Kwa upande mwingine Mh Salleh amewaomba wamiliki wa mifungo mbalimbali katika mtaa huo kuhakikisha wanawafungia mifungo yao ili kuepusha kero kwa wananchi
Image
MAMA ATELEKEZEWA WATOTO WATANO NA BABA WA FAMILIA. Watoto Mama mmoja ametelekezwa pamoja watoto wake watano na mme wake baada ya kumuomba pesa ya matumizi. Akisimulia kisa hicho mama huyo amesema amesikitishwa na kitendo ch mme wake kuikimbia familia kwa jambo la kuombwa pesa ya matumizi hali ambayo imemlazimu kuwa na mzigo mkubwa wa kulea familia pekee yake. Nao majirani wa familia hiyo wamesikitishwa na kitendo cha mwanamme huyo kuitelekeza familia yake. Hata hivyo Radio Sengerema imemtafuta msaidizi wa sheria wilayani sengerema bwn James Sendama ambapo amesema kuwa jukumu la kutunza familia ni la baba na mama katika familia. Aidha bwn Sendama amesema mpaka sasa jumla ya wanawake 18 wilayani sengerema wametelekezwa na waume zao chanzo kikiwa ni kushindwa kutunza familia Deborah Maisa/Emmanuel Twimanye                                  
Image
MBOGA MBOGA ZAGEUKA DHAHABU SENGEREMA mboga mboga Biashara ya mboga  za majani imegeuka   dhahabu tena katika masoko mmbalimbali Wilayani Sengerema  Mkoani Mwanza . Biashara ya mboga hizo  hivi karibuni  watumiaji wengi walisuasia kuitumia kwa madai kuwa  zinadaiwa kuhatarisha maisha ya watu huku  zikidaiwa  kuwa  na  mdudu mtu. Radio Sengerema imeongea na baadhi ya watumiaji wa mboga hizo wamesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuitumia huku wengine  wakisema hawaezi kutumia mboga hiyo  kutokana na   hofu ya kupoteza maisha. Mboga   za   majani   zimekuwa    kimbilio  kwa  watanzania wengi  husasani   wenye maisha ya chini  katika familia zao .      Na Emmanuel Twimanye
Image
KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA KUPITIA ANGA YA JAPANI. Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini J apan . Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang. Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani Rex Tillerson ametoa wito kwa China na Urusi kuchukua hatua za moja kwa moja dhidi ya Pyongyang , huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi. China na Urusi lazima zionyeshe kwamba zimechoshwa na hatua ya Korea Kaskazini kuendelea kufanyia majaribio makombora yake kwa kuichukulia hatua ya moja kwa moja. Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni ,likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika
Image
AJALI YAJERUHI WATU 18 basi la King Msukuma Watu zaidi ya 18 wamefikishwa katika hospitali Teule  ya Wilaya ya Sengerema baada ya basi la king Msukuma kupinduka katika kata ya Katunguru wilaya ya sengerema wakati  likimkwepa mwendesha bajaji barabarani ndipo lilipoyumba na kuanguka. Baadhi ya majeruhi wakiwa hospitali teule ya wilaya ya sengerema wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha bajaji  kutopisha barabarani na dereva ndipo alipolazimika  kuikwepa bajaji hiyo ndipo basi hilo lilipopinduka.  Akithibitisha kupokelewa kwa majeruhi hao muuguzi wa zamu wa hospital hiyo Beatrice Emanueli amesema kwa sasa majeruhi wanaendelea vizuri tofauti na walivyowapokea. Kutokana na kutokea kwa ajali hiyo Dereva  aliyekuwa akiendesha gari hilo la king Msukuma ametokomea kusikojulikana. Na Said Mahera