SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUMALIZA KERO YA MAJI SAFI NA SALAMA
waziri wa Tanzania Kassim Majaliwa |
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji
safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini
zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Amesema
serikali kupitia kampeni ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtua mama ndoo,
itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na
salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa
wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema,
Bicha na Bereko akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za
kikazi.
Waziri Kassimu
amesema kwa sasa Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu, vifupi
pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali
nchini yakiwemo na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo
karibu na makazi yao
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote
watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi
na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.
Aidha Mh.
Majaliwa ameagiza wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu ya
pili ndipo waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh. trilioni
moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado
havijaunganishiwa nishati hiyo.
Comments
Post a Comment