KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA KUPITIA ANGA YA JAPANI.
Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu
kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa
kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang.
Jaribio hilo linakuja siku chache tu
baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi
ya Korea Kaskazini.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa marekani Rex Tillerson ametoa wito
kwa China na Urusi kuchukua hatua za moja kwa moja dhidi ya Pyongyang, huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja jaribio hilo la hivi
punde kuwa ni kitendo cha kuudhi.
China na Urusi lazima zionyeshe kwamba
zimechoshwa na hatua ya Korea Kaskazini kuendelea kufanyia majaribio makombora
yake kwa kuichukulia hatua ya moja kwa moja.
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa
jaribio hilo la hivi karibuni ,likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea
kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang.
Comments
Post a Comment