WATAKAOPANDA MAZAO MAREFU NDANI YA MAMLAKA YA MJI WA SENGEREMA FAINI YA SHILINGI LAKI MBILI
Related image
MAZAO YA MAHINDI
Mwenyekiti    wa    Mamlaka   ya     Mji     Mdogo    Mjini Sengerema     Bwn Richand Buluma amewatangazia kiama watu ambao watapanda mazao marefu ndani ya mamlaka ya  mji wa Sengerema msimu huu wa kilimo.
Hayo ameyasema wakati akiongea na Radio Sengerema mapema hii leo bwn Buluma amewataka wananchi kutokujihusisha na kilimo hicho katika maeneo ya mjini.
Hata hivyo Bwn Buluma ameeleza kuwa watakaokiuka  agizo hilo  watatozwa faini ya shilingi laki mbili 200,000 akishindwa kulipa faini hiyo atafikishwa mahakamani na atafungwa miezi 6 jela.
Kufuatia tamko hilo Diwani wa kata ya Nyatukala Mh Salleh Msabaah amewaomba wananchi wake kuachana na kulima mazao marefu katika maeneo yao kwani ni kinyume cha  sheria.
Kwa upande mwingine Mh Salleh amewaomba wamiliki wa mifungo mbalimbali katika mtaa huo kuhakikisha wanawafungia mifungo yao ili kuepusha kero kwa wananchi.
Hata hivyo diwani huyo amewataka wananchi kuzingatia maagizo hayo   vinginevyo sheria itachukua mkondo wake kwa wale watakaokaidi agizo hilo.

Na Said Mahera. 

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA