Rais Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422.
Rais Magufuli |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli,
leo amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo mbali
mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.
Tukio hilo
ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjni,
limehudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa na mafisa wa Jeshi nchini
pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha.
Kabla ya
kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli amekagua gwaride
maalum, na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi
kwenye masomo yao.
Tukio hilo
la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni la kwanza
kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.
Comments
Post a Comment