UKOSEFU WA HUDUMA
ZA AFYA ZAWATESA WANANCHI
ZAHANATI |
Wananchi wa
kijiji cha Butonga kata
ya Igulumuki wilayani Sengerema
wamelazimika kutembea
umbali mrefu ili kupata
huduma za matibabu Kutokana na ukosefu
wa zahanati katika kijiji hicho .
Hayo yamebainishwa
na mwenyekiti wa kijiji
hicho bwana Thobias Shija Isangu wakati akizungumza
na Radio Sengerema na kusema kuwa hali ya
huduma ya afya sio rafiki kwani wananchi hao
wanalazimika kutembea umbali
mrefu ,kufuata huduma za afya katika zahanati
ya kijiji jirani cha Igulumuki ambapo
hali
hiyo inapelekea kuhatarisha maisha
yao.
Hata hivyo
Bwana Isangu
ameongeza kuwa kwa sasa
wanamajengo ya zahanati lakini
wanahitaji msaada wa kutosha ili waweze kukamilisha
ujenzi wa zahanati hiyo na kuondokana na adha inayowakibili kwa
muda mrefu sasa.
Na Enosy Mashiba
Comments
Post a Comment