Pongezi kwa rais Magufuli
Rais Dkt John Pombe Magufuli |
Mchunganji wa kanisa la
AGAPE lililopo Shinyanga Mch, Moses Maduhu ameipongeza serikali ya muungano
wa Tanzania ikiongozwa na Rais John Pombe Magufuri kuboresha elimu
nchi kwa kuhakikisha inawapa kipaumbele watoto wa kike ili kufikia malengo
yake..
Hayo ameyaeleza kwenye
mahafari ya tatu ya darasa la saba katika shule ya mchepuo wa kiingereza Sayuni
na kudai kuwa serikali ya awamu ya
tano imezidi kutatua changamoto hususani
katika sekta ya elimu.
Pia amewaomba wahitimu
hao kuepuka vikwazo ambavyo watakutanavyo kwani vitawafanya kutotimiza malengo
yao pia nao wazazi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa watoto.
Awali akijibu lisala
iliyosomwa na Goodluck James ambayo shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali licha ya kuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mithiani ya kuhitimu.
Nao wahitimu wamesema watahakikisha wanazingatia ushauri
wa mgeni rasmi.
Mchungaji Mose Maduhu ameahidi kutatua changamoto
hizo ili kuhakikisha shule hiyo inaendelea kufanya vizuri kwa wanafunzi wa
shule hiyo.
Shule ya Sayuni English
Medium school inayomilikiwa na kanisa la FPCT ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na
wanafunzi 64 kwa sasa ina wanafunzi 287 na walimu 16.
Comments
Post a Comment