KILABELA YAIMALISHA ULINZI
SILAHA |
Balozi wa
mtaa wa Kilabera B , kata ya
Nyatukala wilayani Sengerema mkoani
Mwanza Bi, SPESIOZER PAUL amesema
wanaendelea kushirikiana na Jeshi
la polisi ili kuimarisha ulinzi katika
eneo hilo.
Balozi huyo amesema hayo wakati
akizungumza na Radio Sengerema
na kusema kuwa hali
ya usalama katika mtaa
huo ni shwari
kutokana na juhudi
wanazozifanya za kushirikiana
na jeshi la polisi na kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano.
Pia balozi
huyo ameeongeza kuwa wanahitaji ulinzi
shirikishi ili kuzuia uharibifu wa aina yoyote katika
eneo hilo na
hata maeneo mengine
kwa ujumla.
Aidha bi, Spesiozer amewaasa
wazazi na walezi kutambulisha
wageni wao wanaokuja
katika eneo hilo
ili kuepukana na mwingiliano wa watu mbalimbali kwani itawasaidia
kuwabaini watu wanaoingia bila
kufuata utaratibu wa mtaa
huo.
Na Enosy Mashiba
Comments
Post a Comment