MBWA ASABABISHA KIFO SENGEREMA.
Mbwa
picha ya mtandao
Mtoto  mmoja amefariki dunia baada ya kung’atwa na mbwa katika kijiji cha Ibondo kata ya Ibondo Wilaya Sengerema mkoani mwanza.
Mtoto huyo amefahamika kwa  majina ALPHONCE SIKITU (8) aliyekuwa akisoma darasa la kwanza shule ya msingi Ibondo  kata ya Ibondo  wilayani  hapa.  
Akisimulia kisa hicho bibi wa mtoto huyo Bi  Helena Shubalu      ameeleza kilichotokea mpaka    kupelekea mtoto alphonce   kupoteza maisha.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya Ibondo alipokuwa  akisoma mtoto huyo Mwl  Emmanueli Mashili amesikitishwa na kifo cha  mtoto huyo kwani alikuwa akihudhuria darasani kama kawaida licha ya kuwa hakupewa taarifa ya kung’atwa na mbwa.

Naye diwani wa kata hiyo Mathias Mashauri amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wamiliki wa mbwa kuhakikisha wanawachanja mbwa wao chanjo ya kuondoa sumu mwilini.


Matukio ya watu kung’atwa na mbwa yamekuwa yakiendelea kutokea na hili ni tukio la pili kutokea katika kata ya Ibondo hali ambayo imekuwa ikisababisha  kupoteza maisha.
Na Said mahera.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA