AGIZO BODABODA
piki piki(Boda boda) |
Waendesha pikipiki Maarufu kama bodaboda wilayani Sengerema
mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kubeba watoto walio chini ya umri wa miaka tisa kwa kuwa ni makosa kwani
watoto hao hawamudu kusafirishwa wakiwa peke yao bila uangalizi wowote.
Kauli hiyo imetolewa na
mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki wilayani Sengerema Bwn,Joseph Emmanuel Augustine katika
mahojiano na Radio Sengerema ambapo amesema hii ni sheria ya nchi na ni kosa
kubwa kubeba mtoto kwenye pikipiki bila kuwepo
mwangalizi.
Katika hatua nyingine Bwn,Augustine amesema ni vyema jamii
nzima kutoa ushirikiano wa kutoa elimu ,na kuwaomba wandesha pikipiki kufuata
sheria kwani vitu vingi wamepitia ikiwemo sheria ya kuwa na kofia mbili ngumu.
Na Elisha Magege.
Comments
Post a Comment