UDHALILISHAJI WAMFIKISHA MAHAKAMANI
Image result for PICHA YA NYUNDO
Mtu  mmoja  amefikishwa  katika  mahakama   ya   wilaya   ya  sengerema  mkoani  mwanza  kwa  tuhuma   ya  udhalilishaji.
Akisoma  shitaka   linalomkabili   mbele   ya   hakimu   wa  mahakama  hiyo  Bi  Monica   Ndyekobora  ,Mwendesha  mashitaka  wa  jeshi   la  polisi  INSPECTA  SLIVESTA  MWAISEJE,amemtaja   mshitakiwa   kuwa  ni  MWITA   TULETWA  mwenye   umri  wa   miaka  18   mkazi  wa Nkome   Geita.
 INSPECTA    MWAISEJE  amesema   kuwa  mshitakiwa  anashitakiwa   kwa   kosa  la  udhalilishaji  kinyume   na   kifungu  namba  135   cha   kanuni   ya  adhabu   sura   ya   16,  kuwa  mshitakiwa  MWITA   TULETWA   anashitakiwa  mnamo  septemba  11   mwaka   huu   majira   ya   saa  10:00   jioni  huko  katika  kisiwa  cha  Zilagula  wilayani  Sengerema  mkoani   Mwanza  kwa   makusudi  na   isivyo   halali  kumshika msichana ambaye   jina  lake  limehifadhiwa  sehemu za mwili wake bila  lidhaa   yake.

Hata    hivyo   mshitakiwa   amekana   kutenda   kosa  hilo  na   mshitakiwa   amerudishwa   rumande  kwa   kushindwa   kutimiza  masharti  ya   mahakama   hadi  octobar  03   mwaka   huu  kesi   hiyo   itatajwa   kwa   maelezo   ya   awali   mahakamani   hapo.
Na Joyce Rollingstone.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA