UVUVI HARAMU WAGEUKA KAA LA MOTO KUTOKOMEZWA
Nyavu haramu zikiteketezwa kwa moto |
Juhudi za kupambana na uvuvi haramu zimeonekana kutozaa matunda
katika ziwa victoria wilayani sengerema mkoani mwanza na hivyo kutishia ustawi
wa halmashauri ya buchosa ambayo zaidi ya asilimia 80 ya mapato yake ya ndani
yanatokana na sekta ya uvuvi.
Wakizungumza wakati wa kikao cha dharura cha baraza la
madiwani la halmashauri ya buchosa,baadhi ya madiwani wamewanyoshea vidole
wataalam waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya uvuvi kwa kuwa ni kikwazo
kwenye kutokomeza uvuvi haramu.
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru ) wa
wilaya ya sengerema Bwn,Protas Sambagi
amekiri kutofanikiwa kwa juhudi za kukomesha uvuvi haramu huku akitaja sababu
kubwa kuwa rushwa.
Akizungumzia hali hiyo,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Buchosa
Bwn,Crispian Luanda amesema
kuwa hatua zimeanza kuchukuliwa kwa baadhi ya wataalam wa uvuvi wanaonyoshewa
vidole.
Kikao cha dharura cha halmashauri ya Buchosa kimeidhinisha
hesabu za halmashauri hiyo kwa kipindi kinachoishia juni 30 mwaka huu,huku
ikijivunia kupata hati safi kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Na Elisha Magege
Comments
Post a Comment