MAHAKAMANI KISA NYAVU
HARAMU
Watu watatu
wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma ya
kupatikana na nyavu haramu.
Akisoma shitaka
linalowakabili mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bi,Subira Mashambo
mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspecta Sylvesta Mwaiseje amewataja
watuhumiwa kuwa ni Edwin Michael mwenye
umri wa miaka 35 mkazi wa mkolani Mwanza Ernest Manyecha (62) mkazi wa
Ukiliguru Misungwi na Fitina Juma (65) mkazi wa Mkomba Busisi.
Inspecta Mwaiseje
amesema kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la kupatikana
na nyavu haramu kinyume na kifungu namba 66 kifungu kidogo cha kwanza A na
kifungu kidogo cha 4 cha kanuni ya uvuvi kuwa washitakiwa wote kwa pamoja
wanashitakiwa mnamo septemba 23 mwaka huu majira ya 07:00 mchana huko katika
maeneo ya Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwa pamoja walipatikana na
nyavu haramu moja aina ya kokoro kinyume cha sheria.
Hata hivyo washitakiwa
wote kwa pamoja wamekana kutenda kosa hilo na washitakiwa wamerudisha rumande
kwa kushindwa kutimiza masharti ya mahakama hadi novemba 5mwaka huu kesi hiyo
itatajwa kwa maelezo ya awali mahakamani hapo.
Na Joyce Rollingstone
Comments
Post a Comment