WAKULIMA WAPATIWA
PEMBEJEO ZA KILIMO
Mkulima |
Wakulima wa zao la pamba
Wilayani Sengerema
wametakiwa kuendelea kujiandikisha ili kupatiwa pembejeo za kilimo kwa kuwa
zoezi hilo bado linaendelea katika vijiji vyote kwa wakulima wa zao hilo.
Akizungumza na Radio
Sengerema Afisa kilimo Ushirika na Umwagiliaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Sengerema Bwn,Simon Butera amesema
zeozi hilo linaendelea kwa wakulima wote wa zao hilo.
Akielezea hasara za
wakulima hao kutojiandikisha amesema hawata pata pembejeo za kilimo kama
vile mbegu na dawa za kupulizia wadudu.
Hivi karibuni
Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi ambae pia ni mbunge wa jimbo la
Buchosa Dkt;Charles Tizeba katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo lake amesisisitiza
jambo
hilo la kujiandiisha huku akiwataka wananchi kuwa na tabia ya
kutunza mazao.
Aidha Bwn;Butera amesema
zoezi hilo linafanywa chini ya usimamizi wa mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh, Emmanuel Kipole hivyo amewataka
wananchi kutokuwa na shaka na jambo hilo na wajitokeze kujiandikisha kwa wingi.
Na;Elisha Magege
Comments
Post a Comment