Kamati
za shule simamieni mahudhurio ya
wanafunzi “Aron Laiza”
wanafunzi |
Halmashauri ya wilaya
ya Sengerema imesema haitasita kuwachukulia hatua wazazi watakaoshindwa
kuwapeleka watoto shule.
Hayo yamesemwa na
katibu tawala wilaya ya Sengerema BWN ARON LAIZA kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Sengerema katika Hafla ya wiki ya elimu ya watu wazima ambayo yamefanika katika
shule ya msingi Ibondo wilayani Sengerema.
Amesema kamati za shule
zisimamie mahudhurio ya wanafunzi na endapo mzazi atabainika kukwamisha
maendeleo ya mwananfunzi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kupelekwa
mahakamani.
Kwa upande wake Kaimu
Afisa elimu ya watu wazima wilaya ya Sengerema
Bwn Deogratius F Munema
amesema katika elimu ya watu wazima kunachangamoto nyingi zinazo pelekea
kushindwa kufikia malengo waliojiwekea
Hata hivyo maadhimisho
hayo yamefikia kilele ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kisomo katika ulimwengu
wa sayansi na teknolijia kwa maendeleo ya nchi
Deborah Maisa.
Comments
Post a Comment