MABOMBA YAPO ILA MAJI HAYATOKI TUNATESEKA MNO"WANANCHI"
Wakazi
wa mjini Sengerema mkoa wa Mwanza wameilalamikia idara ya maji kwa kukosa maji
wiki ya pili sasa na hawajui tatizo nini hali ambayo imewalazimu kutumia maji
ambayo si safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Wananchi
hao wamesema hawajui tatizo hilo litachukua muda gani kwani mpaka sasa wanapata
usumbufu mkubwa kupata huduma hiyo muhimu.
Kufuatia
hali hiyo Radio Sengerema imemtafuta Meneja wa maji Mjini Sengerema Eng,Christopher Kiwone amekiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa mpaka sasa wanalifanyia kazi hivyo muda
sio mrefu huduma hiyo itarejeshwa.
Aidha
wananchi wameitaka mamlaka husika kulitatua tatizo haraka iwezekanavyo kwani
imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi mjini Sengerema wanaotumia maji ya bomba.
Na Deborah Maisa
Tatizo la idara ya maji ya Sengerema, hawatoi taarifa kwa wananchi kuwajulisha tatizo ni nini na litachukua mda gani.Maji ni mhimu,nyumbani bora umeme ukatike kuliko maji, hakuna alternative ya maji, wawe serious na nafasi zao, kama bili watu wanalipa na service charge ikiwemo, asa hatujui ni ubovu gani uliopo unaochukua zaidi ya wiki 2 sasa
ReplyDelete