NYAVU HARAMU
ZAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU 3.
nyavu haramu za uvuvi |
Watu watatu
wamefikishwa katika mahakama
ya wilaya ya
sengerema mkoani mwanza
kwa tuhuma ya
kupatikana na nyavu
haramu aina ya
timba.
Akisoma shitaka
linalowakabili mbele ya
hakimu wa mahakama
hiyo BI MONIKA
NDYEKOBORA ,mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi INSPECTA
SLIVESTA MWAISEJE ,amewataja
washitakiwa kuwa ni
MASUMBUKO GEREVASI mwenye
umri wa miaka
45 dereva, OMARY TWENTIY
mwenye umri wa
miaka 67, na RAMADHANI
ISSA mwenye umri
wa miaka 25
Wote ni wakazi
wa kijiji cha Nyakarilo wilayani Sengerema.
INSPECTA MWAISEJE
amesema kuwa washitakiwa
wanashitakiwa kwa kosa
la kupatikana na
nyavu haramu kinyume
na kifungu namba
66 kifungu kidogo
cha (1) A na
kifungu kidogo cha
4 cha kanuni
za uvuvi ya
mwaka 2009 kinachotokana na
kifungu namba 57
cha sheria ya
uvuvi namba 22
ya mwaka 2003
kuwa washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa mnamo
septemba 15 mwaka
huu majira ya
saa 6:00 mchana
huko katika kijiji
cha nyamirilo wilayani
sengerema mkoani mwanza
walipatikana na nyavu
haramu 5 aina
ya timba.
Hata hivyo
washitakiwa wote kwa
pamoja wamekana kutenda
kosa hilo na
washitakiwa wako nje
kwa kutimiza masharti
ya mahakama hadi
octobar 16 mwaka
huu kesi hiyo
itatajwa kwa maelezo
ya awali mahakamani
hapo.
JOYCE
ROLLINGSTONE
Comments
Post a Comment