WAKULIMA WILAYANI MISUNGWI WAPEWA MAFUNZO YA
KUTUMIA HATI MILIKI.
Jembe |
Wakulima wa kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi
mkoani Mwanza wamepewa mafunzo ya
namna kutumia hati miliki za mashamba za kimila kwa lengo la kuchukulia
mikopo ili kujiendeleza kimaisha.
Akizungumzia lengo la mafunzo hayo meneja wa Mulabika
ambao ndiyo wanaotoa mafunzo hayo Makame Juma amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia
wakulima hao kujikwamua kimaisha kwa kupata mikopo kwa kutumia hati hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Misungwi Fredrick
Nyoka amesema kuwa kati ya vijiji 113 katika wilaya hiyo ni vijiji viwili
ambavyo vilichaguliwa katika mpango huo ambayo ni Kasololo na Matare Mnamo mwaka
2012.
Nao baadhi ya wakulima waliohudhuria
katika mafunzo hayo wameshukuru kuanzishwa kwa mpango huo na kwamba utawasaidia
kujikwamua kimaisha.
Na Veronica Martine.
Comments
Post a Comment