ULINZI WAIMARISHWA
Kutokana na wizi wa mali za wananchi uliokuwa umeshamili kwa kasi hapo awali  katika kijiji  cha  Butonga   wilayani Sengerema  kwa sasa  wameendelea  kuukomesha   kwa  kushirikiana  na jeshi  la Jadi  maarufu kama sungusungu.

Hayo  yamebainishwa  na mwenyekiti wa kijiji hicho,Bwn Thobias Shija Isangu ambapo amesema kuwa  kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanaishi kwa kuhofia usalama wa mali zao na kuongeza  kuwa  kwa sasa hali ni shwari.

Aidha  mwenyekiti  huyo  ameongeza  kuwa  kwa  sasa  wamekaa  na  jeshi  la  jadi  sungusungu  pamoja  na wananchi  katika  kuimarisha  ulinzi  na  usalama  katika  kijiji  hicho.


Bwn Isangu amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa  na kuwataka waendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili waweze kutokomeza suala hilo.
NA MICHAEL MGOZI. 

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA