AFISA MTENDAJI ATUHUMIWA KUTAFUNA PESA ZA WANANCHI

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyangh’wale kata ya Nyanghwale mkoani Geita bw,Ramadhani Masele Manyero anatuhumiwa  kutafuna pesa za wananchi  sh. Milioni moja zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya ukarabati wa lambo la maji liloharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwaka jana.
Mbele ya kikao cha wananchi kilichohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale bw,Hamim Gwiyama na mbunge wa jimbo hilo bw,Hussein Nassoro ambacho kililenga kutathimini jumla ya fedha zilizochangwa na wananchi pamoja na utekelezaji wake.

Nae Afisa Mtendaji anaetuhumiwa kutafuna pesa za wananchi bw,Ramadhani Nasoro  Manyero amekana mbele ya mkuu wa wilaya hiyo kutumia pesa hizo za wananchi ambazo zilichangwa shilingi 6500 kwa kila kaya.

Hata hivyo mkuu wa wilaya bw,Hamim Gwiyama amemtaka Afisa mtendaji huyo kufika kituo cha polis kilichopo Karuma mapema akiwa na mchanganuo sahihi juu ya matumizi ya pesa hizo baada ya kutoridhishwa  na maelezo yake.


Aidha viongozi wametakiwa kuwa waaminifu kwa wananchi ili  kutatua changamoto zinazowakabili na kuleta maendeleo ndani ya jamii.
Na Anna Elias

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA