SUNGUSUNGU LAWACHAPA VIBOKO WANANCHI
Viongozi wa Jeshi la Jadi wakiwa na Msaidizi wa sheria wilayani sengerema James Sendama (wa pili kutoka kushoto) |
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bungonya kata
ya Nyamazugo Wilayani
Sengerema wamelilalamikia Jeshi la
jadi maarufu
kama Sungusungu
la kijiji hicho
kwa kuwachapa
viboko na kuwatishia kuwafukuza
katika eneo hilo
bila kosa lolote.
Baadhi ya wananchi
ambao ndungu zao wamekumbwa na tukio hilo la kuchapwa viboko
wamesikitishwa na kitendo cha jeshi la jadi kwa maamuzi yake kwa kuwa moja ya jukumu la jeshi la jadi ni kuwakamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua na siyo kuwachapa ovyo viboko.
Wajumbe
wa serikali ya kijiji hicho wamesema kutokana na sakata
hilo viongozi wa kijiji cha Bungonya wanatakiwa
kuwafundisha viongozi wa jeshi la
jadi mipaka ya kazi yao ili kuepuka
kujitia matatani.
Nae Afisa mtendaji wa kijiji cha Bungonya
Bwn,Joseph Makashi Senyenge ameahidi kufanya uchunguzi
ndani ya jeshi la jadi la kikiji chake dhidi ya watu waliowachapa viboko na kuwatishia kuwafukuza
wananchi ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Mwenyekiti wa ulizi wa kijiji hicho Elias Kanyenye Kisununa amesikitishwa zaidi na tuhuma hiyo
inayo waandama huku akidai kuwa atafanya uchunguzi ili kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ndani ya jeshi
la jadi kwa kuwa havivumiliki wala havikubalika
kamwe katika jamii.
Kwa
upande wake Msaidizi wa kisheria Wilayani Sengerema Bwn,James
Sendama amelaani
tukio hilo huku kwa kuwa kuwachapa viboko wananchi ni kinyume na
haki za binadamu.
Tukio la kuchapwa
viboko na kutishiwa kufukuzwa
wananchi na jeshi la jadi katika kijiji cha Bungonya
limesababisha kuibua maswali mengi miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho.
Na Emmanuel Twimanye
Comments
Post a Comment