MFUMO UPIMAJI WA VIWANJA WAZINDULIWA
KIWANJA |
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza kwa kushirikiana na kampuni ya Amboni
Land Consalt imeamua kuanzisha mfumo wa upimaji wa viwanja kwa lengo la kuwaelimisha wananchi pamoja na kutumia mfumo
wa hati miliki na namba za kudumu za viwanja.
Akitoa elimu hiyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo
Bw,Rweikiza katika kikao
kilichofanyika katika kata ya Ibisabageni wilayani Sengerema, amewataka wananchi kutokuwa na shaka juu ya mfumo huo kwa
kusema kuwa upimaji huo hauhusiki na kubomolewa kwa nyumba zao.
Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Ibisabageni Bw,Henry Kakele amewaomba wananchi kuwa na subira na
kuwahakikishia kwamba ombi lao litafika
panapo husika.
Hatahivyo Mwenyekiti amehitimisha kikao
kwa kuwaomba wananchi wote mitaa yote
miwili Busisi Road na Ibisabageni,kuteuwa wajumbe wawili kila mtaa watakaounda
kamati ya upimaji huo.
Na
THOBIAS NGUBILA
Comments
Post a Comment