Posts

Showing posts from November, 2017

SHULE YA MSINGI BULYANGELE KUFUNGULIWA 2018

Shule ya msingi  Bulyangele iliyopo katika kata ya Kasungamile  Wilayani Sengerema   inatarajiwa  kufunguliwa mwaka  2018 ili   kuondoa usumbufu wa watoto kutembea  umbali  mrefu kwenda  shuleni. Hali hiyo imekuja  baada ya    Wananchi wa kijiji cha  Ilekanilo kata ya Kasungamile    kukukubaliana kuwa ifikapo  Januari  mwaka  2018    shule hiyo ifunguliwe . Mwenyekiti   wa kijiji cha Ilekanilo   Bwana Fikiri Yakobo Ruhusa  amesema katika bajeti  ya  serikali ya kijiji hicho   kuna miradi  mingi ya shughuli za  maendeleo ambayo  inahitaji kutekelezwa  hivyo  amewaomba  wananchi   kushikamana  ili     ikamilike miradi  hiyo. Na Charles Sungura.

TISHIO LA FISI GEITA AJERUHI WATU 3

Image
Watu watatu  wameshambuliwa  na fisi na kujeruhiwa    sehemu mbalimbali za miili yao   katika kijiji cha Idoselo Kata ya Lwezela Mkoani Geita .   Afisa mtendaji wa kijiji cha Idoselo Bwn  Samson Kachimu Walwa    amethibitisha kutokea kwa tukio   hilo  na kusema kuwa kundi la fisi hao wamevamia katika baadhi ya familia mkoani humo  kwa lengo la kutafuta mbuzi  ndipo watu hao waliposhambuliwa na fisi hao. Bwn,Walwa amesema kuwa majeruhi wamelazwa katika hospitali ya  Mkoa  wa   Geita  kwa matibabu zaidi. Na Emmanuel Twimanye

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KISA UBAKAJI WA MTOTO WA MIAKA 7 SENGEREMA

Image
Mtu   mmoja  amefikishwa  katika   mahakama ya wilaya ya Sengerema  Mkoani   Mwanza  kwa   tuhuma   ya  ubakaji. Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Monica Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi insipekta Sylivester Mwaiseje amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Robert Pamo   mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Nyamililo wilayani Sengerema mkoani humo. Mwaiseje amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo November 11 mwaka huu majira ya saa 4 katika kijiji cha kijiweni kilichopo wilayani   Sengerema ambapo  alimbaka mtoto ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka saba. Mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na chapili {e} na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu. Mshitakiwa amekiri kosa pamoja na maelezo ya awali ya kosa hilo na amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka  thelathini 30 jela.  Na  HAPPYNESS PAUL  

KIAMA CHATANGAZWA KWA WANAOAJIRI WATOTO CHINI YA MIAKA 18

Wananchi wanaowajiri watoto kufanya kazi za ndani wametakiwa kuzijua sheri za watoto kabla ya kuwapatia ajira na  kuhakikisha kazi wanazowapa haziwadhuru kiafya, kielimu na katika ukuaji wao. Hayo yamebainishwa na Afisa ustawi wa jamii wilayani  sengerema mkaoani mwanza Nyanjige Julius Nkwabi wakati akizungumza na Redio Sengerema. Afisa ustawi amesema kuwa   wanapaswa kutambua kuwa wanapoajiri mtoto aliyechini ya umri wa miaka 18 watambue kuwa huyo ni mtoto na alindwe kwa mujibu wa sheria. Hata   hivyo amewataka watoto pamoja na wazazi wa watoto hao kutoa   taarifa   katika ofisi za ustawi wa jamii ama ofisi za serikali za mitaa pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili . Na Neema Hussin.

MJI WA SENGEREMA WAANZA KUIMARIKA KWA USAFI

Image
Hatimae mji wa Sengerema umeonekana kuwa katika hali ya usafi kutokana na kampuni iliyokabidhiwa kufanya kazi hiyo kuzoa  taka kwa wakati kwa baadhi ya maeneo mjini hapa. Wafanya usafi wakifanya usafi mjini Sengerema Taka hizo zimeonekana kupungua kutokana na kampuni iliyo kuwepo kushindwa kufanya kazi hiyo ,na kukabidhiwa Kampuni ya mazingira ya  Social  Environmental Workers Association (SEWA) ambayo imeonekana kuwa na kasi zaidi katika shuguli hiyo. Akitolea ufafanuzi  wa maeneo ambayo hayajafikiwa kwa wakati, mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw n.Ndaturu Yohana amesema sababu kubwa ni kutokana na upungufu wa vitendea kazi, na kuwaomba wananchi  kuwa na subira kwani  ndani ya muda usiozidi siku 14 maeneo yote yatakuwa katika hali ya usafi mjini Sengerema. Aidha baadhi ya wananchi wamewaomba  wafanyausafi hao kuwafikia katika maeneo yalio nje ya mji ,hususani katika msimu huu wa masika. Vilevile Bwn.Yohana  amewaomba wananchi kila moja kuujua umuhimu wa kutunza maz

RADIO SENGEREMA YAJITOLEA KUCHANGIA DAMU

Image
Meneja  mkuu wa kituo cha  habari na mawasiliano    Sengerema Telecentre   Bw,Sosteness Tangaro   ameongoza  wafanyakazi  wa kituo hicho pamoja na baadhi ya wananchi Wilayani Sengerema   kujitolea kuchangia  damu  ili kuokoa maisha ya watu  wenye uhitaji wa damu.  Zoezi hilo  la  uchangiaji   wa damu   limefanyika katika  Ukumbi  wa kituo cha habari na mawasiliano  Sengerema Telecentre. Mara baada ya   zoezi  hilo   Bwn, Tangaro  amesema   viongozi  pamoja na wafanyakazi wa Radio Sengerema    wameamua kujitolea  kuchangia damu   kutokana  na  umoja  na  kuona  umuhimu  wa  kusaidia  watu   wenye uhitaji wa damu  walioko   Hospitalini. Kwa  upande  wake Dakitari  ambae  pia, ni  mratibu  wa   damu  Salama  wilaya  ya  Sengerema  Bwn, Selestini   Visenti  Muga   amefurahishwa     na  uamuzi  wa  viongozi ,wafanyakazi  wa Radio Sengerema pamoja na wananchi     kujitoa  kuchangia  damu. Na Thobias Ngubila.

KILA KAYA YAHIMIZWA KUJENGA CHOO MTAA WA IGOGO SENGEREMA

Image
Wananchi wametakiwa kuhakikisha kila kaya wanakuwa na choo kuepuka  kutokea kwa magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu hususani kipindi hiki cha mvua.   Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Bwn Goodluck Daud ambapo amesema kuwa,wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuchimba choo  kutokana na hali ya eneo husika. Bwn Daud ameongeza kuwa, kwa sasa mwitkio ni mzuri kwani kila kaya wamekuwa wakijenga vyoo vya muda wakati wakijipanga kujenga choo cha kudumu. Hata hivyo, wananchi wametakiwa kutambua kuwa suala kuwa na sehemu iliyosafi ili kulinda afya za familia zao kwani ndio chanzo cha uboreshaji wa mazingira na afya ya jamii. Na Michael Mgozi.

VITENDO VYA KIHALIFU VYAWATESA ILEKANILO SENGEREMA

Image
Wananchi wa kijiji cha  Ilekanilo  kata ya Kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza  wamekubaliana  kufanya   ulinzi  shirikishi  ili kudhibiti  matukio  ya uhalifu kijijini  hapo. Makubaliano hayo yamefanyika kwenye kikao cha kubaini wahalifu kufuatia tukio la ujambazi lililofanyika kijijini hapo kwa pamoja wameweka mikakati ya ulinzi ili kuhakikisha tukio hilo halitokei tena. Akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti wa kijiji cha Ilekanilo  Bwana Fikiri Yakobo Ruhusa amewataka wananchi kuwa na subira na kushirikiana katika kutokomeza matukio ya ujambazi Naye Diwani wa kata ya Kasungamile Mh,Julias Ndekeja amekubaliana na upigaji wa kura za siri ili kuwabaini watu wanaosumbua kwa matukio ya uhalifu pia amewataka wananchi kushikamana katika kupambana na matukio ya uhalifu. Ndekeja   amesema kutokana na matukio ya ujambazi kuongezeka katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismassi na mwaka mpya wananchi wametakiwa kuongeza umakini kwa wageni mara wanapoona

WAPIGA DEBE WAENDELEA KUKAIDI AGIZO STEND KUU SENGEREMA

Image
Kufuatia baadhi wa Wapiga debe kuendelea kukaidi agizo lilitolewa na serikali la kuondoka katika stend kuu ya Magari mjini Sengerema Afisa Usalama barabarani wilayani Sengerema Inspecta Hamis Wembo amewataka kuondoka mara moja. Insepcta Wembo ameyasema hayo wakati akizungumza na Radio Sengerema ambapo amesema mpaka sasa baadhi ya wapiga debe wamekamatwa kwa kushindwa kutii agizo hilo na tayari wamefikishwa mahakamani. Afisa usalama barabarani amewataka wapiga debe hao  waangalie njia nyingine ya kutafuta  riziki katika maisha na kwamba wakiwa wahalifu watachukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wao wapiga debe wamesema kuwa agizo hilo linawaumiza na kuiomba serikali iwaangalie kwa mara ya pili kwani hawana sehemu ya kwenda. Hata hivyo inspekta Wembo amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kupambana na wale wote watakaovunja utaratibu uliowekwa,na kwamba zoezi hili sio  kwa Wilaya ya Sengerema pekee  yake bali ni kwa Taifa zima. Na Glorius Balele.

TABIA YA UNYANG'ANYI YAIBUKA WILAYANI SENGEREMA

Image
Watu wanaodhaniwa kuwa wanyag’anyi  wamekuwa wakifanyia unyang’anyi wa vitu mbalimbali akina mama wanaotumia njia ya Misheni kwenda Kizungwangoma wilayani Sengerema. Akithibitisha kuwepo kwa hali hiyo Mwenyekiti wa kitongoji cha Kizungwangoma Bw Kwiligwa Metusela Katolyo alipokuwa akizungumuza na Radio Sengerema ambapo amekiri kuwepo kwa hali hiyo kitongoji hicho. Bw Katolyo amesema kuwa matukio hayo yamekuwepo na kusema watu wanaohusika na matukio hayo ni watu wa vitongoji jirani hivyo wameanzisha msako wa siri ili kuwabaini wahusika hao. Kwa upande wake bi Monika Joseph ambaye ni mhanga wa tukio amesema amefanyiwa tukio hilo na kundi la wanyang’anyi na kuelezea jinsi alivyovyamiwa na watu hao. Aidha Mwenyekiti wa kitogonji hicho amewaomba wananchi wasijichukulie sheria mkononi pindi watakapowakamata wahalifu hao. Na Tumain John.

UKATILI WA KIJINSIA INATAKIWA UKOMESHWE

Image
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo,ubakaji,pamoja na mimba za utotoni, dawati la jinsia  katika kituo cha polisi wilayani Sengerema limeamua kutoa elimu kwa wazazi na jamii kwa ujumla ili kukomesha vitendo hivyo. Hayo yamebainishwa na bi MARTHA SLYVESTA CHACHA ambaye ni msimamizi wa dawati la jinsia kituo cha polisi wilaya ya Sengerema ambapo amesema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na polisi jamii katika kuelimisha wazazi. Bi CHAHA amebainisha kuwa jumla ya kesi mia moja na mbili (102) zimeripotiwa katika dawati hilo kati ya mwaka 2016/2017,ambapo kesi zote zimeripotiwa na tayari zefikishwa mahakamani. Hata hivyo kutokana na elimu wanayotoa kwa jamii, vitendo vya ukatili wa kinjinsia vimeonekana kuripotiwa kituoni hapo kwa kiwango kikubwa ikilinganisha na miaka ya nyuma ambapo jamii ilikuwa haina mwamko wa kuripoti vitendo hivyo. Na Deborah Maisa          

ZAHANATI NNE ZAFUNGIWA KWA MIEZI 6 SENGEREMA

Image
Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia,wazee na watoto imezifungia zahanati nne kutoendelea na utoaji wa huduma za Afya kwa muda wa miezi sita  katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza. Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya  Sengerema Dkt, Peter Mau wakati akizungumza na Radio Sengerema  Ofisini kwake. Amesema kuwa zahanati ambazo zimefungwa ni pamoja na zahanati ya kanisa la AIC (T )Africa Inland Church Of Tanzania Pastoret ya katunguru,Mama Dispensar ,KMT Dispensar na HURUMA Dispensar zilizopo mjini Sengerema. Ameleza sababu zilizo pelekea Zahanati hizo kufungwa ni pamoja na kuwa na wauguzi wasio na sifa za utabibu,upungufu wa majengo na baadhi ya zahanati hizo kushindwa kulipia  ada ya mwaka inayotambuliwa na  wizara ya Afya hapa nchini . Zoezi la kufungia zahanati na vituo vya Afya visivyozingatia vigezo kwa mjibu wa Wizara ya Afya limetajwa kuwa ni zoezi endelevu,lengo ikiwa ni kuhakikisha huduma  bora za kiafya  zinatole

SAKATA LA MBWA KUNG'ATA WATU LAENDELEA SENGEREMA

Image
Kufuatia  matukio ya watu kung’twa na mbwa wilayani Sengerema, Kaimu Afisa mifugo na uvuvi wilayani Sengerema Bwn Nestory Mmbare ,anatarajia kutuma watalaamu kwa ajili ya kufanya tathmini ili kuwaangamiza mbwa wanaozagaa mitaani kwani wamiliki wake wameshindwa kuwafungia ndani. Akiongea na Radio Sengerema ofisini kwake amesema kuwa,wanapopata taarifa kutoka kwa uongozi wa kata kuwa wamesababisha madhara hutuma watalaam kwa ajili ya tathmini na badae hatua za kuwaua huanza mara moja.. Aidha, Bwn Mmbare ameongeza kuwa,wazazi wanapaswa kuwa waangalifu kwa watoto ili kuepusha madhara kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wamiliki kuwakana mbwa wao pindi wanawapong’ata mtu. Kaimu Afisa mifugo na Uvuvi,amekiri kupokea  malalamiko kutoka kwa baadhi ya kata ikiwemo kijiji cha Kahumulo kata ya Nyamatongo wilayani hapa na kutuma watalaamu kwa ajili ya kushugulikia suala hilo. Hata hivyo,amewataka wamiliki wa mbwa kuwatengea bajeti ya chakula ili kuepusha kuzagaa mitaani kwan

RADIO SENGEREMA YAWASAIDIA WAJASILIAMALI WALIOTISHIWA KUONDOLEWA GEITA

Image
Wajasiliamali  wanaojishughulisha  na upondaji kokoto katika mlima uliopo eneo la I Banda kata ya Kanyala wilayani   Geita mkoani Geita   wameipongeza Radio Sengerema kwa  kuwasaidia kuendelea kufanya kazi katika   mlima huo licha ya viongozi wa eneo hilo kutaka kuwaondoa. Pongezi hizo wamezitoa wakati Radio Sengerema ilipotembelea katika mlima huo kwa lengo la kujua kama shughuli zinaendelea za upondaji kokoto kwa wajasiliamali hao. Kwa upande wake Mwenyekiti wa wajasiliamali wa eneo hilo a nae ameipongeza  Radio Sengerema kwa   kufanikisha  kumaliza  mgogoro  huo baina ya wajasiliamali na viongozi wa eneo hilo. Mwaka jana viongozi wa eneo la Ibanda walilazimika kuitisha mkutano kwa lengo la kuwahamisha wajasiliamali hao kwa kigezo cha kupata mwekezaji ambaye alihitaji kuwekeza katika mlima huo.   Na Said Mahera. 

KAYA 38 ZATOZWA FAINI KWA KUKOSA CHOO NA BAFU SENGEREMA

Image
Jumla  ya     kaya  38   katika   mtaa  wa  maduka matatu  kata  ya  Nyatukala  wilayani  sengerema  zimetozwa  faini  ya  shililngi  elfu  kumi  kwa  kwa kila  kaya  kwa  kutokuwa  na  choo  na  bafuu.    Hayo  yamebainishwa   na  mwenyekiti  wa  mtaa  huo  bwana,  PASCHAL   LUJIGILWA  wakati  akihitimisha   msako  wa  kuwabaini  wananchi  wasiokuwa  na choo  na  bafu  na  kusema kuwa  wameamua  kufanya   msako huo   kutokana  na  baadhi  ya   wakazi  wa  eneo  hilo  kuishi  bila  kuwa  na  choo  pamoja  na  bafu  hali  iliyopelekea  kuwatoza  faini  ya  shilingi  elfu  kumi  kwa  kila  mmoja   ili   kukomesha  suala  hilo. Hata  hivyo  wananchi  wa  mtaa  huo  wameunga  mkono  juhudi  zinazofanywa  na  mwenyekiti  huyo  kwani  tatizo  la  kutokuwa  na choo pamoja  na  bafu kwa  baadhi  ya  wananchi  limekuwa  ni  sugu  sasa  Aidha   katika  hatua  nyingine mwenyekiti  huyo  amesema  kuwa   tozo  iliyotolewa  na  wananchi  hao  ambao  wamebainika  kutokuwa  na  choo  

UNDP YAWASILISHA RIPORT YA MAJARIBIO YA AWALI YA MRADI WA UZALISHAJI GESI ASILIA HALMASHAURI YA SENGEREMA

Image
Majaribio   ya    awali  ya    Mradi    wa     uzalishaji    wa   Gesi  asilia  kupitia ufadhiri  wa   shirika  la    United     Nations  Development  Programme   (UNDP)  umeonekana  kuwa  na    mafanikio   makubwa  kwa  jamii  ya  wilaya  ya  Sengerema   kutokana   kupunguza   tatizo  la  kukata   miti   ovyo na   kupunguza  uharibifu   wa   Mazingira. TIMU  KUTOKA UNDP PAMOJA NA WATAALAM WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUWASILISHA RIPORT YA MAJARIBIO YA AWALI YA MRADI WA UZALISHAJI WA GESI ASILIA KATIKA HALMASHAURI YA SENGEREMA. Mradi  huo  umeingia    wilayani  Sengerema   mnamo  mwaka  2015 katika  kijiji  cha  Nyampande  wilayani  hapa  ambapo  umeonekana  kuwa  na  mwitikio   mkubwa   kwa  jamii   kuhitaji  kutumia  mradi  huo. Akizungumzia  mradi  huo  mwezeshaji  wa  mradi   UNDP Joseph  Malkia kwa  niaba  ya  shirika  la  UNDP ameeleza  jinsi    jamii  ilivyoupokea  mradi  huo. Kwa   upande  wake   Afisa    mazingira   wa  wilaya    ya  Sengerema  B

SIKU 2 ZATOLEWA KWA WAPIGA DEBE KUONDOKA STENDI MJINI SENGEREMA

Image
Jeshi la  polisi  kitengo cha usalama barabarani Wilayani Sengerema   limetoa muda wa  siku  mbili  kwa  wapiga debe  waliopo katika kituo kikuu  cha  mabasi wilaya Sengerema kuondoka  mara moja   na  atakaye kiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.   Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Insipecta Hamis Wembo ambapo    amesema agizo hilo   ni  maelekezo yaliyotolewa  kutoka ngazi ya juu ya serikali kuwa kuwepo kwa wapiga debe wengi ni chanzo cha usumbufu kwa abiria na kwamba maelekezo hayo yasipo fanyiwa kazi hatua za kisheria zitachukuliwa. Kwa upande wao baadhi ya   wapiga debe wamelipokea agizo hilo vizuri  na  kuahidi  kuwa  watalifanyia kazi kama walivyo agizwa  ,huku wengine   wakilipokea kinyonge kutokana na kwamba  sehemu  hiyo ilikuwa ni moja ya kujipatia riziki katika maisha yao. Sambamba na hayo inspector Wembo amesisitiza suala la usalama barabarani  kwa kuwataka madereva  wa vyombo vya moto   makini wawapo safarini ili k

KANISA LA GMC LAZUA KIZAA ZAA SENGEREMA

Mwenyekiti  wa  mtaa  wa  maduka  matatu  kata  ya  Nyatukara   wilayani  Sengerema   bwana   PASCHAL     LUJIGILWA,  amelionya   vikali   kanisa  la  GMC  liliopo   katika   mtaa   huo   kwa   madai   ya   utovu  wa  nidhamu. Mwenyekiti  huyo  ametoa  kauli  hiyo  katika  mukutano  wa  hadhara  uliofanyika  katika   mtaa  huo    na  kusema  kuwa  wameshindwa  kuwaheshimu  wananchi  wa  eneo  hilo  wakati  wakiwa  wanafanya  mkuutano  huku  wao  wakiwa  wanaendelea  kufanya  mazoezi  ya  kwaya  hali   iliyopelekea   kushindwa  kuelewana  katika  mkuutano  huo. Katika  hatua  nyingine  wananchi  wa  eneo  hilo  wamekerwa   na   tabia   kwani  limekuwa  ni  tatizo   la  mda  mrefu   mpaka   sasa  huku  wengi  wao  wakimpongeza   mwenyekiti  wa  mtaa  huo  kwa  hatua   aliyoichukuwa  ya   kuwaonywa  kwani  pengine  itakuwa  ni  suluhisho   la  kudumu. Hata  hivyo   kwa  upande  wake   mama  mchungaji  wa  kanisa  hilo  la  GMC   ambaye  hakujitambulisha  kwa  jina  amekiri 

JAMII YAHIMIZWA KUSAFISHA MAZINGIRA SENGEREMA

Image
Wananchi wametakiwa kuzingatia suala la usafi wa mazingira na kuachana na dhana ya kusubiri kusukumwa na viongozi ili  kuepusha magonjwa ya mlipuko  katika kipindi hiki cha mvua. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano wilayani sengerema,Bwn Goodluck Daud wakati akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake. Bwn,Daud ameongeza kuwa,kipindi hiki cha mvua ni hatarishi kwani kuna uwezekano mkubwa wakutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Pia amewataka wananchi kulinda na kuishi katika hali ya usafi ili waimalishe afya za familia kwa ujumla. Hata hivyo,amefafanua kuwa jamii imekuwa na mwitikio mkubwa katika suala nzima la usafi na wanaokaidi hufikishwa katika vyomba vya sheria kwa hatua zaidi. Na Michael Mgozi

MITIHAN DARASA LA NNE LEO YAANZA NCHI NZIMA

Image
Jumla ya wananfunzi   elfu   kumi na moja na arobaini   wa  darasa la nne   wameanza   kufanya  mithiani yao     ya    kujipima Kitaifa  leo   Wilayani  Sengerema  Mkoani  mwanza. Hayo yameelenza na  afisa elimu  wilaya ya Sengerema bwn Osca Kapinga amesema  mitihani hiyo  imeanza  vizuri  na kusema kuwa kati ya wanafunzi  elfu kumi  na  moja  na arobaini  wavulana  ni  elfu tano miambili themanini na saba  na wasichana ni  elfu tano mia saba hamsini na  tatu.     Mithiani ya  upimaji  kitaifa kwa  wanafunzi wa darasa la nne nchini kote inatarajiwa kumalizika    Novemba  23 mwaka huu  huku   mitihani ya  kidato cha pili ikitarajiwa kumalizika Novemba 24 mwaka  huu. Na Said Mahera

MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AIPONGEZA RADIO SENGEREMA

Image
Kutokana na vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii vinavyoruka kupitia kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecenter  Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh Emmanuel Kipole amewashukuru watumishi  wa wa kituo hiki kwa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu ya haki ya mtuhumiwa awapo katika vyombo vya dola wilayani Sengerema. Mh Kipole amewashukuru watumishi hao kupitia makala ya Jicho la jamii inayorushwa na Radio Sengerema na kudai kuwa kipindi hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa jamii husika hivyo wananchi wazingatie elimu hiyo kwani ina manufaa kwao. Aidha amewataka raia kutambua kuwa mtu yeyote anapaswa kuzitambua haki zake pindi anapokuwa katika vyombo vya dola na kuongeza kuwa kutuhumiwa ni jambo la kila mtu hivyo wazingatie ni hatua zipi zinazotakiwa kuchukuliwa na sio kuwabishia askari pindi wanapowakamata wakidai kutenda kosa. Mh,Kipole  amewaomba wananchi wanaoishi vijiji kuacha kutetereka pindi wanapotuhumiwa kutenda kosa kwani mtuhumiwa yeyote anawajib

MBWA WAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA SENGEREMA

Image
Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Martina John anaekadiliwa  kuwa na umri wa miaka 50 ameng’atwa na mbwa na kumjeruhi goti la mguu wa kushoto katika kata ya mwabaruhi  wilayani Sengerema. Akiongea na Radio Sengerema mama huyo amesema kuwa alikuwa akipita njiani akielekea shambani ndipo mbwa waliokuwa kwenye mji walimkimbia na kuanza kumshambulia. Radio senerema imemtafuta mmiliki wa mbwa hao Bi.EVA PHILIMON  amekiri mbwa wake kumng’ata mama huyo na ameahidi kumpeleka katika huduma za matibabu. Awali balozi  wa mtaa wa Kanyamwanza bw.SIMON MPUYA amekuwa akiwatahadharisha wamiliki wa mbwa kuwafungia nyakati za mchana licha ya baadhi yao kuendelea kukiuka maagizo hayo. Mwenyekiti wa mtaa wa Kanyamwanza bw.INNOCENT SEGEREDI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa wamiliki wa mbwa kuwafungia ndani ya kibanda nyakati za mchana ili kunusuru matukio ya mbwa kuwashambulia watu. Na Anna Elias

MTOTO APIGWA NA BABA YAKE KISHA KUFUNGIWA NDANI KWA SIKU 4 KISA KUCHUMA MAEMBE SENGEREMA

Image
Mtoto mwenye umri wa miaka 10 aliyetambulika kwa jina la Simon   Emmanuel  amepigwa   na   baba  yake  kisha kufungiwa ndani  ya  nyumba  kwa siku  nne kwa  kosa   kuchuma  maembe ,huku akiwa amezuiliwa  kwenda kuchuma maembe na mzazi wake. Baada ya hapo   Radio  Sengerema  imefunga safari   hadi  katika Hospitali   Teule ya Wilaya  ya  Sengerema ambako mtoto huyo anapatiwa matibabu na kuongea na mtoto huyo na kuthibisha  kupigwa na mzazi huyo kwa kosa la kuchuma maembe. Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kanyamwanza amethibitisha kutokea kwa ukatili huo na kuwaasa wazazi , walezi na jamii kwa ujumla kuacha mara moja  ukatili dhidi ya watoto. Mganga mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya sengerema  Dkt ,Mery  Jose  amethibitisha kupokea kwa mtoto huyo ambapo amesema mguu wa mtoto huyo umevunjika na anaendelea na matibabu.  Na Enock Makala/Anna Elias

ELIMU KWA WAFUGAJI WA KUKU SENGEREMA.

Image
Wafugaji   wa   kuku   wilayani   Sengerema   wametakiwa   kuwapatia   chanjo      kuku   wao   kwa   kufuata     maelekezo   sahihi   kutoka   kwa    watalamu   wa   mifugo . Hayo  yamebainishwa  na  mwezeshaji  wa shirika  la Farmers Empowerment Intietive  ( FEI )   linalojihusisha  na  utoaji  elimu kwa   wakulima  na wafugaji   ambae  pia  ni  afisa  mifugo  wilaya  ya Sengerema       bwana  GEORGE  NKUBA  ,katika  mkuutano  uliofanyika  katika  ukumbi  wa kituo  cha habari  na  mawasiliano  Sengerema  Telesentre   na kusema kuwa  lengo  la kuendesha  semina hiyo ni kuwasaidia wafugaji  waweze kutumia  mfumo mzuri wa ufugaji na usio hitaji  mtaji mkubwa. Hata  hivyo  bwana   NKUBA    amewataka wafugaji  wa kuku  kuwapatia chanjo   kuku wao   kwa   kufuata   maelekezo  wanayopewa  na  watalaamu  ili  kuondokana  na  magonjwa  yasio  ya  lazima kwa  mifugo. Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa  shirika  hilo  la  FEI  bwana ,ZEPHANIA  LUTOBEKA   amesema  kuwa lengo  l
WASTANI WA BEI YA MAZAO                    HALMASHAURI YA SENGEREMA MKOANI MWANZA.              JAMII YA MAZAO JINA LA ZAO KIPIMO BEI NAFAKA Mahindi Debe 11,000 -12,000 Mchele Kilo 2,000 Mtama Debe 12,000 Mawele Debe 13,000 Ulezi Kilo 2,000 JAMII YA KUNDE Maharage Kilo 2,000 Kunde Kilo 2,000 Njugumawe Kilo 3,000 Choroko Kilo 2,000 Njegere Kilo 3,000 Dengu Kilo 3,000 MAZAO YA MIZIZI Viazi mviringo Kilo 1,000 Mihogo mibichi Fungu 1,000-2,000 Viazi vitamu Fungu 1,000-2,000 Mihogo mikavu  (Makopa/Udaga) Debe 10,000-11,000