ZAHANATI NNE ZAFUNGIWA KWA MIEZI 6 SENGEREMA
Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia,wazee
na watoto imezifungia zahanati nne kutoendelea na utoaji wa huduma za Afya kwa
muda wa miezi sita katika halmashauri ya
wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa halmashauri
ya Wilaya ya Sengerema Dkt, Peter Mau wakati akizungumza na Radio
Sengerema Ofisini kwake.
Amesema kuwa zahanati ambazo zimefungwa
ni pamoja na zahanati ya kanisa la AIC (T )Africa Inland Church Of Tanzania
Pastoret ya katunguru,Mama Dispensar ,KMT Dispensar na HURUMA Dispensar zilizopo
mjini Sengerema.
Ameleza sababu zilizo pelekea Zahanati
hizo kufungwa ni pamoja na kuwa na wauguzi wasio na sifa za utabibu,upungufu wa
majengo na baadhi ya zahanati hizo kushindwa kulipia ada ya mwaka inayotambuliwa na wizara ya Afya hapa nchini .
Zoezi la kufungia zahanati na vituo vya
Afya visivyozingatia vigezo kwa mjibu wa Wizara ya Afya limetajwa kuwa ni zoezi
endelevu,lengo ikiwa ni kuhakikisha huduma
bora za kiafya zinatolewa hapa
Nchini.
Na Katemi Lenatus
Comments
Post a Comment