MTOTO APIGWA NA BABA YAKE KISHA KUFUNGIWA NDANI KWA SIKU 4 KISA KUCHUMA MAEMBE SENGEREMA
Mtoto mwenye umri wa
miaka 10 aliyetambulika kwa jina la Simon Emmanuel
amepigwa na baba yake
kisha kufungiwa ndani ya
nyumba kwa siku nne kwa
kosa kuchuma maembe ,huku akiwa amezuiliwa kwenda kuchuma maembe na mzazi wake.
Baada
ya hapo Radio Sengerema imefunga safari hadi
katika Hospitali Teule
ya Wilaya ya Sengerema ambako mtoto huyo anapatiwa
matibabu na kuongea na mtoto huyo na kuthibisha
kupigwa na mzazi huyo kwa kosa la kuchuma maembe.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kanyamwanza amethibitisha kutokea kwa ukatili
huo na kuwaasa wazazi , walezi na jamii kwa ujumla kuacha mara moja ukatili dhidi ya watoto.
Mganga
mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya sengerema Dkt ,Mery
Jose amethibitisha kupokea kwa
mtoto huyo ambapo amesema mguu wa mtoto huyo umevunjika na anaendelea na
matibabu.
Na Enock Makala/Anna Elias
Comments
Post a Comment