KILA KAYA YAHIMIZWA KUJENGA CHOO MTAA WA IGOGO SENGEREMA

Wananchi wametakiwa kuhakikisha kila kaya wanakuwa na choo kuepuka  kutokea kwa magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu hususani kipindi hiki cha mvua.
Image result for PICHA YA CHOO 
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Bwn Goodluck Daud ambapo amesema kuwa,wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuchimba choo  kutokana na hali ya eneo husika.


Bwn Daud ameongeza kuwa, kwa sasa mwitkio ni mzuri kwani kila kaya wamekuwa wakijenga vyoo vya muda wakati wakijipanga kujenga choo cha kudumu.



Hata hivyo, wananchi wametakiwa kutambua kuwa suala kuwa na sehemu iliyosafi ili kulinda afya za familia zao kwani ndio chanzo cha uboreshaji wa mazingira na afya ya jamii.
Na Michael Mgozi.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA