UKATILI WA KIJINSIA INATAKIWA UKOMESHWE
Kutokana
na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo,ubakaji,pamoja
na mimba za utotoni, dawati la jinsia katika
kituo cha polisi wilayani Sengerema limeamua kutoa elimu kwa wazazi na jamii
kwa ujumla ili kukomesha vitendo hivyo.
Hayo
yamebainishwa na bi MARTHA SLYVESTA CHACHA ambaye ni msimamizi wa dawati la
jinsia kituo cha polisi wilaya ya Sengerema ambapo amesema wamekuwa
wakishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na polisi jamii katika
kuelimisha wazazi.
Bi
CHAHA amebainisha kuwa jumla ya kesi mia moja na mbili (102) zimeripotiwa
katika dawati hilo kati ya mwaka 2016/2017,ambapo kesi zote zimeripotiwa na tayari
zefikishwa mahakamani.
Hata
hivyo kutokana na elimu wanayotoa kwa jamii, vitendo vya ukatili wa kinjinsia
vimeonekana kuripotiwa kituoni hapo kwa kiwango kikubwa ikilinganisha na miaka
ya nyuma ambapo jamii ilikuwa haina mwamko wa kuripoti vitendo hivyo.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment