SAKATA LA MBWA KUNG'ATA WATU LAENDELEA SENGEREMA
Kufuatia
matukio ya watu kung’twa na mbwa wilayani
Sengerema, Kaimu Afisa mifugo na uvuvi wilayani Sengerema Bwn Nestory Mmbare,anatarajia kutuma watalaamu
kwa ajili ya kufanya tathmini ili kuwaangamiza mbwa wanaozagaa mitaani kwani
wamiliki wake wameshindwa kuwafungia ndani.
Akiongea
na Radio Sengerema ofisini kwake amesema kuwa,wanapopata taarifa kutoka kwa
uongozi wa kata kuwa wamesababisha madhara hutuma watalaam kwa ajili ya tathmini
na badae hatua za kuwaua huanza mara moja..
Aidha,Bwn Mmbare ameongeza kuwa,wazazi
wanapaswa kuwa waangalifu kwa watoto ili kuepusha madhara kwani kumekuwa na
tabia ya baadhi ya wamiliki kuwakana mbwa wao pindi wanawapong’ata mtu.
Kaimu
Afisa mifugo na Uvuvi,amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya kata ikiwemo
kijiji cha Kahumulo kata ya Nyamatongo wilayani hapa na kutuma watalaamu kwa
ajili ya kushugulikia suala hilo.
Hata
hivyo,amewataka wamiliki wa mbwa kuwatengea bajeti ya chakula ili kuepusha
kuzagaa mitaani kwani kutopata chakula ndiyo chanzo kikubwa cha kuwa na mbwa wa
mitaani wanaosababisha madhara kwa binadamu.
Na Michael Mgozi.
Comments
Post a Comment